Ticker

6/recent/ticker-posts

TAMWA-ZNZ Yawapiga Msasa Wadau Wa Kupinga Udhalilishaji Na Ukatili Kwa Wanawake Na Wasichana


Na Tatu Juma Zanzibar,

Chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa Zanzibar kinaendeleza juhudi ya kupambania kutoweka kwa vitendo vya udhalilishaji Zanzibar.

Akizungumza na mwandishi wa habari za mitandaoni huko Ofisini kwao Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja Afisa Programu kutoka chama  hicho Asia Hakimu Makame katika hafla ya mafunzo ya siku mbili ya vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na wasichana yaliyowahusisha viongozi katika jamii Mkoa wa Kaskazini A na B Unguja.

Amesema mafunzo hayo yanalengo la kuwajengea uwezo wa kutambua viashiria vya udhalilishaji katika jamii kwa wanawake na wasichana pamoja na kutoa elimu na  kuzishuhulikia kesi pamoja na kuzirufaisha kutoka hatua moja ama nyengine ili jamii iweze kupata urahisi wa hukumu ya kesi hizo.

Hata hivyo amesema ingawa vitendo vya udhalilishaji wa kujinsia sio tatizo la Zanzibar pekee  hivyo  chama hicho kimeamua kutoa elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja na Pemba kwani kuna vitendo vingi vya udhalilishaji haviripotiwi kwa wakati.

"Suala la udhalilishaji ndio janga la ulimwengu wote lakini kwa hapa Zanzibar Mkoa wa mjini ndio unaoongoza kuripotiwa kila kukicha ndio maana tumeona tufanyie kazi Mkoa wa Kaskazini Unguja na Pemba kwa lengo la kutoa elimu hiyo kwani kuna vitendo vingi vya udhalilishaji kwa uhalisia huwa haviripotiwi kwa wakati"amesema Afisa Asia



Nae muezezeshaji wa mafunzo hayo Dkt. Skujuwa Omar Hamdan amesema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kutoa mafunzo kwa washiriki  hao ni kuungana pamoja katika kuisaidia jamii ili badae iwe ni njia sahihi ya kuelimisha dhidi ya kesi hizo.

"Washiriki wetu wamepata muamko mkubwa kwasababu jamii zao wanazitambua nawao wenyewe wamezidi kupata uelewa juu ya mamna ya kuishi na wahanga na unufaishaji wa kesi za udhalilishaji zinavyofanyika ndani ya familia,ndani ya jamii zao wenyewe,natumai wataenda kuwafundisha wenzao kile ambacho wamekipata"amesema Dkt.Skujua



Nao baadhi ya wadau walioshiriki mafunzo hayo wameeleza kuwa, elimu waliyoipata itawasaidia kufanya kazi kwa mashirikiano ya karibu, kuanzia ngazi ya jamii hadi mahakamani, ili kuhakikisha vita dhidi ya udhalilishaji inafanikiwa na jamii inakuwa salama.

Aidha wamesema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa mpana katika kupamabana na vitendo hivyo na namna ya kumsaidia mwananchi aliyepatwa na vitendo hivyo.

Miongoni mwa walioshiriki mafunzo hayo ni pamoja  na Masheha,wasaidizi wa sheria,waratibu wa shehia,viongozi wa vikundi mbali mbali,walimu wa madrasa,Maafsa ngazi za wilaya,Polisi Dawati, Mkono kwa mkono,Mahakimu pamoja na DPP.

Mradi huo wa miezi nane unaotambulika kwa jina la Tunaweza pamoja unaotekelezwa na Chama cha waandishi wahabari wanawake Tamwa Zanzibar kwa kushirikiana na UN WOMEN pamoja na ubalozi wa Norway.

Post a Comment

0 Comments