Ticker

6/recent/ticker-posts

Uthubutu Wa Wanawake Katika Kugombania Nafasi Za Uongozi



Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:

Kwa miaka mingi, nafasi za uongozi zimekuwa zikihusishwa zaidi na wanaume, hali iliyowafanya wanawake wengi kuogopa kujitokeza kugombea au kushika nafasi za juu za maamuzi. 

Hata hivyo, hali imeanza kubadilika kutokana na wanawake jasiri na wenye uthubutu zimeanza kusikika ndani na nje ya Tanzania, zikionesha kuwa mwanamke ana uwezo sawa wa kuongoza, kusimamia maendeleo, na kuchochea mabadiliko chanya katika jamii.

Kwa mujibu wa Takwimu za Umoja wa Mataifa (UN Women, 2024), idadi ya wanawake wanaoshika nafasi za kisiasa duniani imeongezeka kutoka asilimia 11 mwaka 1995 hadi asilimia 26% mwaka 2024 ikionesha ishara kwamba uthubutu wa wanawake unazidi kuleta matokeo makubwa.

Salama Masingwa ni mwanamke aliyethubutu kugombea nafasi ya udiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM katika wadi ya Kinuni wilaya ya Magharib B katika vipindi viwili, licha ya upinzani mkali wa kijinsia alioupata wakati wa kugombea nafasi hiyo lakini aliweza kupambana na dhana kwamba "nafasi za uongozi si za wanaume pekee hivyo kila mmoja ana haki ya kushika hizo"

“Nilipoamua kugombea, wengi walisema nitashindwa, lakini niliamua kuthibitisha kuwa uongozi hauangalii jinsia, bali ni uwezo.”

Rahima Said Abdalla ni mwanasiasa kijana kutoka mjini Zanzibar, anayejulikana kwa kampeni zake za uwazi, uadilifu na uwakilishi wa wanawake ,vijana kupitia chama cha Chaumma ligombea nafasi ya uwakilishi katika jimbo la kwerekwe huku akiamini kwamba mwanamke anaweza kufanya maendeleo makubwa katika jamii kuliko mwanaume.

Kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya Zanzibar (2001), vijana wanawake wanapaswa kupewa nafasi za maamuzi, jambo ambalo Rahima amelisimamia kwa vitendo kupitia harakati zake.

Harusi Mpatani ni mwanasheria wakili wa kujitegemea kutoka shirika la mswaada wa kisheria na haki za binadamu ZALHO ambaye aliona haja ya kuwahamasisha wanawake kushiriki katika kugombea nafasi mabimbali za uongozi baada ya kushuhudia wanawake wengi hawana sauti kwenye maamuzi ya kijamii.  

Aliweza kutumia taaluma yake kusaidia wanawake kupata haki katika masuala ya ardhi na mirathi, huku akiongoza kampeni ya kushajihisha wanawake kugombea nafasi za uongozi inayohamasisha ushiriki wa wanawake kwenye uongozi.

Alisema imani yake kubwa ni kuwa utekelezaji wa Mkataba wa CEDAW (1979) na Azimio la Beijing (1995) ndiyo njia ya kuimarisha usawa wa kijinsia katika 

Asia Fadhili Makame ni muhamasishaji wa jamii kutoka shehia ya Mkokotoni Wilaya ya Kaskazin A ambaye aliona umuhimu wa kuhamasisha jamii juu ya ushiriki Sawa wa kugombea nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi ili kuweza kuondokana na dhana ya uongozi ni kwa ajili ya wanaume pekee. Alisema kuwa uongozi si heshima tu bali ni fursa ya kuleta mabadiliko na maendeleo bora katika jamii na nchi kwa ujumla kupitia viongozi wanawake.

Alisema kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za maendeleo ikiwemo Chama Cha Wandishi wa habari wanawake Tanzania kw aupande wa Zanzibar (TAMWA ZNZ) amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wanawake kutokata tamaa licha ya changamoto za kijamii na kiuchumi zinazojitokeza kwa wanawake hao.

Hivyo kupitia Sera na Matamko Yanayounga Mkono Ushiriki wa Wanawake

Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (Zanzibar, 2001) inasisitiza kuwa usawa wa fursa kwa wanawake na wanaume katika uongozi na maamuzi.

Pamoja na Mkataba wa CEDAW (1979) Unalenga kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake katika nyanja zote za maisha, ikiwemo siasa hivyo hatuna budi kutekeleza mikataba hiyo kivitendo.

Hata hivyo alisema Azimio la Beijing (1995) linahimiza nchi wanachama kuongeza uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi kwani nchi nyingi zinazokuwa na viongozi wanawake hujenga maendeleo bora ya nchi na taifa kwa ujumla.

Alisema pia Agenda 2030 (SDG 5) lengo namba tano linahimiza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika sekta zote kupitia mikataba hiyo hakuna budi kushiriki kikamilifu katika nafasi za uongozi na maamuzi.

Uthubutu wa wanawake katika kugombea nafasi za uongozi siyo hadithi ya bahati, bali ni matokeo ya ujasiri, elimu, na uelewa wa haki zao.

Ni jukumu la jamii, serikali, na taasisi zote kuhakikisha wanawake wanapata mazingira rafiki ya kugombea, kuongoza, na kufanya maamuzi.

Kama ilivyosemwa katika Tamko la Beijing,

“Maendeleo ya jamii hayatawezekana bila ushiriki kamili wa wanawake katika kila ngazi ya maamuzi.

Post a Comment

0 Comments