Ticker

6/recent/ticker-posts

Nyumba Za Gharama Nafuu Kujengwa Zanzibar


Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) limesema linampango wa kujenga nyumba za kuwapangisha watu wenye kipato cha chini katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba.                                                                                                                                                  

Kauli hiyo imetolewa mwisho wa wiki na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Mwanaisha Ali Said wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Shirika hilo Darajani, Unguja. Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetenga ardhi ya akiba kwaajili ya Maendeleo hivyo Shirika litatumia fursa hiyo kujenga nyumba za kupangisha na kuuza kwa wananchi mbali mbali kwaajili ya kuleta makaazi bora. 

Mkurugenzi Mwanaisha amesema ZHC kwasasa imeanza kujenga nyumba za kuuza katika eneo la Mombasa kwa Mchina lakini hata mwananchi mwenyewe kipato cha chini anaweza kununua kutokana na utaratibu mzuri ambao ZHC imepanga kuziuza nyumba hizo. Alieleza kwamba nyumba hizo zitauzwa kwa Wazanzibari waliyopo ndani na nje ya nchi, muhimu mtu afuate taratibu za manunuzi zilizoekwa na Shirika hilo.

Alifahamisha ZHC itauza nyumba hizo kwa njia tatu, aidha njia kulipa pesa zote kwa pamoja, au njia ya kulipa pesa kwa awamu nne au kwa njia ya benki (mogeji hauzi) " Mogeji hauzi ( Morgage house) ni njia ambayo mtu anazungumza na benki hivyo sisi Shirika tunapokea pesa kutoka benki na lakini mteja yeye atafunga mkataba na benki kwaajili ya kukatwa pesa za nyumba hiyo" Alisema 

Mwanaisha Aliezea kwamba ZHC iko tayari kupokea pesa za nyumba zinazojengwa Mombasa kwa Mchina kwani ujenzi umeshaanza tangu Machi 2023 na utamalizika baada ya miezi 15 kuanzia mwezi huyo.

Amesema nyumba hizo zitauzwa bei tofauti kutokana na idadi ya vyumba kwani kuna nyumba za vyumba viwili zitauzwa tsh. Milioni 136 na nyumba ya vyumba vitatu zitauzwa milioni 153, bei hizo bila vati (VAT). 
Nyumba zinazojengwa na Shirika la Nyumba Zanzibar( ZHC) eneo la Mombasa kwa Mchina UngujaAidha mkurugenzi Mwanaisha alizungumzia suali la mazingira ya usafi katika eneo la nyumba hizo, alisema dhamana ya usafi, ZHC itamkabidhi Bodi ya Kondominia ambayo ni taasisi moja wapo ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi ndio itakayobeba dhamana ya kuweka Mazingira safi katika maeneo ya 2 hizo.                                                                                   
Mwisho Mkurugenzi Mwanaisha amemshukuru Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuwaunga mkono katika gharama za Ujenzi wa nyumba hizo kwani bila ya kupata msaada kutoka Serikali kuu Shirika lisingeweza. 

Ujenzi wa Nyumba za Mombasa kwa Mchina utagharimu Tsh. Bilioni 9.8 ambapo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa Tsh bilioni 6.8 na Shirika la Nyumba Zanzibar ( ZHC) limetoa Tsh Bilioni 3.

Post a Comment

0 Comments