Na Najjat Omar:
Mei 30,2024
Wizara Ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Waziri Wa Habari,
Vijana, Utamaduni Na Michezo Tabia Maulid Mwita amewasilisha Makadirio Ya Mapato Na Matumizi Ya Fedha Kwa
Mwaka 2024/2025 amesema kuwa mwaka 2023/2024 jumla ya vyombo vya Habari za ra
45 vimekaguliwa Unguja na Pemba ni 14.
Katika
hotuba yake Waziri Tabia amesema Zanzibar imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa
mashindano makubwa ya mpira wa miguu Afrika yanayoitwa CAF African Schools
Football Championship. Ni mashindano yaliyozikutanisha timu 14 (timu saba za
Wanaume na timu saba za Wanaweke) za vijana wenye umri wa chini wa miaka 15
kutoka mataifa mbali mbali Afrika.
Kwa upande
wa Tanzania bara kupitia kwenye Bajeti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari imeeleza hadi kufikia mwaka 2024 imesajili vituo vya
Runinga 133, Redio 446, kebo 117 huku magazeti yakiwa 672.
Kuwepo wa
takwimu hizo ni dhahiri kwamba ukuwaji wa tasnia ya Habari kwa sasa inakuwa kwa kasi kubwa licha ya
wingi wa vyombo vya habari ni sawa na kuwepo kwa vingi waaandishi wa Habari
pia.
Licha hivyo
utafiti uliofanyika mwaka 2019 na Baraza la Habari Tanzania – MCT unaonesha
waandishi wa Habari Wanawake wengi wanaandika na kuripoti Habari za afya
,kilimo na jinsia.
Salma Abdul
ni Mhariri Mkuu wa Radio ya Uyui Fm iliyopo Mkoani Tabora licha ya kuwa mhariri
Salma pia ni muamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu na mwandishi wa Habari za
michezo amesema waandishi wanawake hawapendi kuandika na kuripoti michezo kwa
sababu kwa upande wa michezo sio tu kujua kuandika bali pia ni kufahamu Elimu
ya kina ya michezo.” Mimi nilipomaliza chuo nilianza kuandika michezo na
nilipata mafunzo kutoka TFF ya uamuzi hivyo najua kanuni,sheria na hata
miongozi ya mpira” Ameendelea kusema kwamba kwa sasa uandishi wa michezo sio kuandika
tu bali ni kuchambua zaidi kwa kina.
Hali hii iko
tofauti kwa Florencia Peter Meneja wa Vipindi kutoka Jembe Fm, radio iliyopo
Mkoani Mwanza anayeongoza wafanyakazi 32 kati ya hao waandishi wa michezo ni
watatu, wawili wanaume na mmoja ni mwanamke.”Waandishi wanawake wanaona kwamba
kuwa mwaandishi wa michezo ni kazi ngumu na ni sehemu ya wanaume jambo ambalo
halina ukweli” Florencia anasema walipoanza kupata mtangazaji wa kike kwenye
vipindi vya michezo wameongeza wasikilizaji.
Ripoti ya
mwaka 2023 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania -
TCU
imeonesha kuwa wanafunzi 261,555 wamehitimu vyuo vikuu kati ya mwaka 2018 hadi
2022 huku kati hao waliosomea Uandishi wa Mawasiliano ya Umma ni 3,634.
Flora
Mwakasala ni Mhariri wa Kilimanjaro Revival Fm redio iliyopo Mkoani Kilimanjaro
akiwa kiongozi ambaye anasimamia wafanyakazi 13 amesema si kwa wafanyakazi tu
bali hata jamii inaona kwamba mwandishi mwanamke kuwa kwenye michezo ni suala
ambalo haliko sahihi “Kuna dhana kwamba Habari za michezo ni wanaume tu sio
Wanawake wanaweza kuandika hio ndio naona ni sababu ambayo kunakuwa na uhaba wa
waandishi Wanawake kwenye upande wa michezo” Ameshauri kuwa ni vyema waandishi
wajue na wajifunze juu ya Elimu na masuala ya michezo licha ya kuwa wanahabari.
Ziada Kilobo
ni Msimamizi wa Uendelevu wa Taasis katika Baraza la Habari Tanzania – MCT
amesema kwa miaka sita sasa Baraza la Habari Tanzania limekuwa likitekeleza
mradi wa kuwawezesha waandishi wa Habari ambao ni viongozi waliopo kwenye
vyumba vya Habari pia kuna utaratibu maalum unaowalea waandishi wa Habari
wachanga ambao wanajikita katika masuala ya kimichezo.”Kwanza ni fursa kwa
mwaandishi mwanamke ambaye amejikita kwenye uandishi ,kwa sababu si wengi
waliojikita huko, kwa kudhani kuwa huko hakuna fursa ila ni ukweli kwamba kwenye
uandishi wa michezo kuna uhaba mkubwa wa waandishi wanawake na hilo tumeliona
na tunalifanyia kazi kwa kuwahamasisha zaidi” Amemaliza Ziada.
Utafiti
uliofanywa na Taasis ya Wanawake wa Afrika kwenye michezo unaonesha waandishi
wa Habari waliopo kwenye vyombo vya Habari wengi wao wamesomea taalum nyengine
na kisha kusomea uamuzi ndipo wanapopata nafasi ya kuwa waandishi na
wachambuzi.
Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake – TAMWA -Z kinatekeleza mradi wa mwaka mmoja
ambapo umewapatia mafunzo waandishi wa Habari 20 Kutoka Unguja na 10 kutoka
Pemba kuleta ushawishi wa kuandika na kuripoti
ujumuishaji wa michezo wa wasichana na Wanawake kwenye sekta ya michezo.
0 Comments