Mjumbe wa Bodi FAWE, Sabrina Omar Abdulla Akimkabidhi vifaa vya Skuli Mmoja wa Wanafunzi wa Skuli ya msingi Tumbatu Uvivini |
Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:
SHIRIKA la Kuwawezesha Wanawake
Kielimu na Kiuchumi Zanzibar (FAWE) limesema litaendelea kuunga mkono
adhima ya serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanapa elimu katika mazingira
mazuri.
Mjumbe wa Bodi ya FAWE Sabrina Omar
Abdulla alisema hayo alipokuwa katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya skuli
kwa wanafunzi wenye mazingira magumunwa ngazi ya msingi na sekondari wa skuli
ya Tumbatu Uvivini.
Alisema kundi kubwa la wanafunzi
hususani wa vijijini hali zao duni hivyo kupitia hatua hiyo itawasaidia kupata
elimu bora kwa maslahi yao ya badae.
Alisema wanafunzi wanapopata
mahitaji yao kwa wakati huwasaidia kuwa imara na kupata faraja hatua
ambayo huwawezesha kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika masoomo yao na
kuiletea nchi maendeleo kupitia nyanja mbalimbali.
Sabrina alisema kabla ya kutoa
msaada huo walifanya utafiti na kuona mahitaji ya watoto hao hivyo hatua hiyo
itawawezesha wanafunzi hao kupata elimu bora na kutimiza ndoto zao.
Alisema taasisi hiyo pamoja na
mambo mengine lakini pia malengo yake ni kuhakikisha kwamba inasaidia watoto
hao ili kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu hivyo wanaamini kwamba sadaka
hiyo itawafariji na kusoma vizuri kama wanafunzi wengine.
Hivyo alitumia fursa hiyo kuwaomba
watu wenyeuwezo kutoa sadaka na kuwasaidia watoto hao kwasababu mahitaji yao
makubwa.
Nae Sheha wa Shehia ya Tumbatu
Uvivini Ngwali Sheha Haji aliwataka wazazi na wadau wengine wa elimu kuunga
mkono jitihada zinazochukuliwa katika kuimarisha upatikanaji wa elimu ili
kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika mazingira mazuri ya kujisomea.
Alisema hatua iliyochukuliwa na
taasisi hiyo ya kuwekeza katika sekta ya elimu ni yakupigiwa mfano kwasababu itasaidia
wanafunzi kuwaweka katika mazingira rafiki ya kujisomea.
“Katika shehia yangu kunawananchi
wanaishi kwa mazingira tofauti wengine hali zao duni za kipato na wengine
mayatima hivyo hupitia wakati mgumu kutokana na kushindwa kumudu sare za skuli
lakini kupatiwa msaada huu utawapa moyo na ari ya kuendelea vyema na masomo
yao,”alisema.
Mbali na hayo aliwataka wazazi na
walezi kuutunza msaada huo waliokabidhiwa ili kuona watoto hao wanasoma katika
mazingira mazuri.
Kwa upande wake Msaidizi Mwalimu
Mkuu wa Skuli hiyo Majaliwa Khamis Juma alisema sare ni nyenzo muhimu za
kujifunzia hivyo hatua hiyo itawafanya wanafunzi hao kujiamini katika masomo
yao.
Alisema taasisi hiyo haikukurupuka
kupeleka msaada huo lakini imeamua kufanya hivyo kutokana na uhalisia wa maisha
duni ya watoto hao.
“Kunabaadhi ya wanafunzi
tunawavumilia huja skuli na nguo za nyumbani na wengine hukatisha masomo
kutokana na kukosa mazingira rafiki ya kujisomea ikiwemo yunifomu hivyo sadaka
hii itawawezesha kufikia malengo yao,”alisema.
Alifahamisha kuwa jitihada
zilizofanywa na taasisi hiyo za kuiunga mkono jitihada za serikali za kuwekeza
katika sekta ya elimu ili kuongeza kiwango cha ufaulu na kufikia malengo ya
kuwa na taifa bora la wasomi.
Baadhi ya wanafunzi waliokabidhiwa
msaada huo walishukuru fawe kwa hatua hiyo kwani itawasaidia kwenda skuli
wakiwa katika mazingira mazuri na kutumia muda huo kuahidi kusoma kwa bidii ili
kufikia malengo yao.
Zaidi ya wanafunzi 52 waliyopo
katika mazingira magumu wa msingi na sekondari kutoka skuli hiyo walikabidhiwa
msaada wa sare za skuli ikiwemo mkoba, viatu, unifomu na vitu vingine kutoka
kwa taasisi ya FAWE.
0 Comments