Ticker

6/recent/ticker-posts

Wandishi Wa Habari Chipkizi Tumieni Kalamu Zenu Vizuri

 


Na Amrat Kombo, Zanzibar

Mjumbe wa Bodi wa Chama cha Wandishi wa Habari Tamwa - Zanzibar  Hawra Shamte  amewataka waandishi wa habari chipkizi kutumia vizuri kalamu zao kwa lengo la kuisaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo udhalilishaji.

Akizungumza katika sharehe za mahafali ya waandishi wa habari chipkizi katika ukumbi wa bima amesema uwepo wa waandishi wenye uweledi itasaidia kuibua matatizo yanayojitokeza kwenye jamii.

Pia alisema  ni vizuri kuishi kwa malengo kwasababu itamsaidia kufanya juhudi katika utendaji wake wa kazi pamoja na kuipaisha tasinia ya habari.

" Ni vizuri mukaishi kwa malengo ya kuwa mwaandishi bora unaeweza kuisaidia jamii hali hii  itasaidia kufanya kazi kwa uwadilifu na ukakamavu na kuacha kufanya kazi kwa ajili ya masilahi ya kupata kitu." alisema 

Khairat Haji ambaye ni Kaimu Afisa Programmu TAMWA -Zanzibar alisema katika hatua za kumarisha uongozi kwa wanawake ,mradi huu ni awamu ya pili .

" Mradi wa kwanza uliwasimamia waandishi vijana 18 kwa 2022 na mwaka 2023 waandish vijana 24 waliopata fursa katika mradi hu wa wanawake na uwongozi." alisema 

Pia alisema katika mradi huo ulikuwa unahitaji kazi 348 na hadi kufikia kazi 347,huku magazeti 47,makala za radio 117 na huku makala za mitandao ya kijamii 187.

Mwandishi wa Habari Mkongwe kutoka Deutsche welle  Zanzibar Salima Said alisema  chama cha waandishi wa habari wanawake imesaidia kuleta mabadiliko makubwa katika jamii ikiwemo kuongezeka kwa ripoti za vitendo vya udhalilishaji.

" Chama cha Waandishi wa Habari Tamwa - Zanzibar walipotoa elimu kwa waandishi wa habari imesaidia kuwasemea wananchi ambao hawana sauti,kuleta mabadiliko ya kubadilishwa kwa sheria,jamii kubadilika pamoja  na kuweza kuripotiwa  tarifa za udhalilishaji." alisema Salama 

Sambamba na hayo alisema  Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake imesaidia kueleza Serikali hadi kuleta mabadiliko katika sekta ya sheria kwa lengo la kueka msaada katika jamii kwa watu ambao wanafanyiwa vitendo vya udhalilishaji.

Naye Mwananchama wa chama hicho Fatma Matulanga amesema chama cha waandishi wa habari kimeandaa mafunzo ya kuwaelewesha wandishi wa habari chipkizi jinsi ya kuandika na kuripoti habari mabalimbali.

" Chama cha Waandishi wa Habari Tamwa -Zanzibari kimeandaa mafunzo haya kwa vijana kwa lengo la kujifunza jinsi ya kuandika habari za wanawake na  uwongozi,kisiasa, kijinsia pamoja na takwimu." alisema 

Pia alisema Chama hicho  kinasaidia kushajihisha wanawake kuingia katika kugombea nafasi mabalimbali za uwongozi kwa lengo la kuweza kutoa maamuzi pamoja na kulinda haki za wanawake na watoto.

" Vijana hawa wamepewa mafunzo hayo na namini watakuwa tayari  kuandika habari za wanawake na watoto pamoja na kuwahabarisha jamii matukio mabalimbali amabayo yanaendelea katika nchi.

Miongoni mwa wahitimu hao Khadija Rashid Nassor  ametoa shukrani kwa chama hicho kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamewasaidia kuibua matatizo  mbalimbali yaliyopo katika jamii amabayo yanarudisha nyuma maendeleo ya wanawake .  

" Tumeweza kujifunza kuwa waandishi wa kisasa pamoja na kuibua matatizo mabalimbali yaliyopo katika jamii ikiwemo mifumo dume,uhaba wa upatikanaji wa huduma za kijamii,utumiaji mbaya wa sheria za kidini.

Sambamba na hayo alisema wameunda kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya habari na mitandao ya kijamii pamoja na kamati ya tathimini na ufatiliaji.

Pia amesema mafanikio mbalimbali wamepata ikiwemo kupatikana kwa eneo la wajasiria mali wenye ulemavu kwa lengo la kutimiza malengo yao.

" kwa upande wa wajasiria mali wa micheweni  walikuwa na ndoto kubwa lakini walikuwa na changamoto ya kupata ufasi yao binafsi na sasa wameweza kukabidhiwa eneo." alisema  

Aidha kupitia mafunzo haya imesaidia viongozi kuweza kufatilia changamoto zinazowakabili wananchi.

Naye miongoni mwa waandishi waliofanya vizuri katika mafunzo hayo Hassan hamza alisema amefurahi kupatiwa mafunzo hayo kwasababu yamesaidia katika kuongeza ujuzi katika sekta hiyo.

Hivyo amewaasa waandishi wenziwe chipkizi kuendeleza mafunzo hayo katika utendaji wao wa kazi kwa lengo la kuwa mwaandishi bora katika jamii.

Post a Comment

0 Comments