Ticker

6/recent/ticker-posts

Bi. Shifaa "Punguzeni Urefu Wa Mahojiano Inapunguza Ladha"


Na Thuwaiba Habibu:

Mwenyekiti wa kamati ya utetezi kutoka Chama Cha Waandishi Wa Habari TAMWA Bi Shifaa Said Hassani amewapongeza waandishi wa habari chipukizi kwa  kuutendea haki mradi wa wanawake na uongozi kwa kufanya kazi kwa kitaalamu zaidi.

Ameyasema hayo  katika sherehe ya mahafali  ya waandishi  wa habari chipukizi  yaliofanyika ukumbi wa bima  Zanzibar alisema waandishi wa habari chipukizi  wameweza kutendea haki mradi wa wanawake na uongozi pamoja na  kuweza kuibua vitu mbalimbali ikiwemo changamoto za wajasiriamali wa Micheweni.

Pia alisema wameandika habari pamoja na makala zenye taaluma na ubunifu kwa kuangalia mikataba ya kikanda na kimataifa.

 "tumezowe kuona makala zinazomuhusu mtu anahojiwa mtu mmoja peke yake lakini wao walitumia vyanzo tofauti tofauti vya habari  na kazi zao ambazo amefanywa ziliandikwa kitaalamu kwani wengine kusubutu kutumia mikataba ya kikanda na kimataifa."

Pia aliwataka waandishi hao wasifanye mahojiano marefu ili kuleta ladha zaidi katika makala zao.

Alisema changamoto ambayo niliona ndani ya makala mulizofanya ni  mohojiano marefu suala ambalo nimenifanya nijilazimishe kusikiliza na kusoma.

Aidha alisema kwa mwaka huu kidogo waandishi wamelisahau kundi la watu wenye ulemavu na kuwataka waandishi wajisongeze karibu na watu hawa kwani hizi ni sauti za wasio sauti

 "Hata kama hatukuwaweka katika makala zetu basi japo tuwafanyie mahojiano na wao wawe miongoni mwa walioshiriki alieleza."

 Nae mjumbe wa bodi ya Tamwa bi Hawra shamte aliwaomba  waandishi hao waweze kuwa ngangari na kutekeleza vigezo vyote vya uandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao Vizio ili kuhakikisha sauti za wanawake, vijana,watoto na watu wenye ulemavu zinasikika.

Alisema munatakiwa kuwa waadilifu na kufuata maelekezo ya uandishi wa habari na tusifanye kazi  kwa kutegemea kitu na tufanye kazi kwa ajili ya kutetea jamii yetu.

Hata hivyo aliwashukuru wahariri na wasimamizi kuwasimamia kufanya utendaji kazi ulio imara.

" Mumeonesha kujitoa na kutuheshimisha kwa kuhakikisha  wanawake wanapata nafasi  wanazo stahiki na naamini kuwa nyinyi ndio wahariri wa baadae".

Nao wahitimu wa mradi huo Berema Suleman Nassor na Nihifadhi Abdallah Issa walitowa shukurani kwa chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa kwa kuweza kuwapatia mafunzo  yaliyoweza kuwafunza namna ya kuandika habari za wanawake na uongozi

Awali walikuwa hawajuwa kitu gani wafanye katika kukamilisha kazi hii lakini kutokana na mafunzo waliopatiwa waliweza kujuwa kuandika hata kwa kutumia mikataba mbali mbali

Vile vile walisema kuna changamoto mbali mbali walizokabiliana na lakini walihakikisha wanazishinda ili kukamiliza kazi hizo.

Post a Comment

0 Comments