Ticker

6/recent/ticker-posts

CECAFA Yaahirisha Mashindano Ya Beach Soccer Zanzibar Ikiwa Tayari Kwa Safari

 


Na Ahmed Abdulla:

Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza kuahirishwa kwa mashindano ya soka la Ufukweni Afrika Mashariki na Kati, yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kati ya Julai 16 hadi 20, 2025, mjini Mombasa, Kenya.

Taarifa hiyo imekuja kwa mshangao, kwani hadi jana, timu ya taifa ya Zanzibar ilikuwa tayari imeagwa rasmi na leo Jumatatu ilikuwa ikitarajiwa kuanza safari kuelekea Mombasa kushiriki mashindano hayo.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Jumapili, Julai 13, 2025, CECAFA imesema mashindano hayo yamesitishwa kufuatia ombi maalum kutoka Serikali ya Kaunti ya Mombasa pamoja na mamlaka za serikali kuu ya Kenya.

“Mashindano haya yamesitishwa kufuatia maombi kutoka Serikali ya Kaunti ya Mombasa na mamlaka husika za kitaifa,” ilieleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA, Auka Gecheo.

Hali hiyo imewaacha wachezaji wa Zanzibar na viongozi wa timu katika sintofahamu, hasa baada ya kukamilisha maandalizi na mipango ya usafiri. Timu hiyo ilikuwa miongoni mwa zile zilizojitayarisha mapema na kufuata taratibu zote muhimu kwa ajili ya mashindano hayo.

CECAFA imesema itatangaza tarehe mpya baada ya kushauriana na Serikali ya Kaunti ya Mombasa ili kuhakikisha mashindano hayo yanaendana na ratiba na mikakati ya maendeleo ya kaunti hiyo.

Kwa mawasiliano zaidi, CECAFA imetoa anwani ya barua pepe: media@cecafaonline.com.


Post a Comment

0 Comments