Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud Akizungumza na Madereva na Maafisa usafirishaji pamoja na maafisa ukaguzi wakati akifungua mafunzo ya usalama Barabarani |
Mkuu wa mkoa Wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amewashauri Wasimamizi na wakaguzi wa miundombinu ya usafiri na usafirishaji kuhakikisha miundombinu hiyo inakuwa imara ili kupunguza ongezeko la ajali za barabarani.
Akifungua mafunzo ya usalama barabarani huko chuo cha Mumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bububu alisema Ongezeko la Ajali za barabarani Zanzibar linatokana na upana wa bara bara zinazojengwa haulingani na idadi ya vyombo vya moto na watumiaji ambapo barabara hizo huwa na msongomano.
“Mara nyingi tunapozungumza kuhusu usafiri na usafirishaji tunaviangalia zaidi vyombo vya vya usafirishaji tunasaha kuwa wakati mwengine miundombinu nayo inaweza kusababisha ajali hivyo nendeni mkaishauri serikali inapofikiria kufanya ujenzi wa marabara izingatie mahitaji ya wakati uliopo” Alisema Ayoub
Alifahamisha kuwa barabara zinazoelekea katika maeneo ya uwekezaji hasa katika mkoa wa kusini Unguja zimezidiwa na harakati nyingi pamoja na ongezeko la wahamiaji na hivyo kuwa chanzo cha ajali za mara kwa mara.
Hata hivyo Ayoub alisema elimu ya usslama barabarani bado inahitajika na kukishukuru chuo cha Taifa cha usafirishaji kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatakuza ufanisi katika taasisi za umma hasa katika sekta ya usafirishaji.
“Niwashukuru NIT kwa kuandaa mafunzo hayo ila fikirieni mafunzo haya zaidi wa taasisi za umma ili kuona madereva wa taasisi za umma wanakuwa na weledi wa hali ya juu” Aliongeza
Mhe Ayoub alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikifanya marekebisho ya sera na sheria ili kuifanya sekta ya usafiri na usafirishaji kuwa salama.
Naye kaimu Makamu Mkuu wa chuo cha Taifa cha Usafirii NIT Dkt. John Mahona alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa nchi nzima kwa watendaji viwanja vya ndege na wakaguzi wa miundo mbinu ya barabara kwa ajili ya usalama wa wananchi.
“Mafunzo haya pia tumewapatia wakaguzi wa barabara kwa sababu huko ndio kwenye changamoto pia wakati wa ujenzi wa barabar” Alise.a Dkt. Mahona
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Usalama barabarani kamishna msaidizi wa polisi LEONARD MACHUMU aliwaomba madereva na watumiaji wengine wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani.
“Tunachoomba kwa wajaenzi wa barabara hizi barabara hizi barabara zijengwe upya kwani barabara nyingi za Zanzibar zimejengwa hazina sehemu za watembea kwa miguu” Alisema Leonard Machumu
Mafunzo hayo y a siku tano amewashirikisha madereva wakuu wa taasisi za umma,wakaguzi wa bara bara na jeshi la polisiReplyForward |
0 Comments