Ticker

6/recent/ticker-posts

Wizara ya Afya Watakiwa Kufanya Kazi Na Waandishi

 

 


Zanzibar,

Na Nafda Hindi:


Wizara ya Afya imeombwa kutoa mashirikiano mazuri kwa waandishi wa habari kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji ripoti  ya elimu ya Afya ya Uzazi kwa wasichana na wanawake wa mjini na vijijini katika ukumbi wa Kificho Mwanakwerekwe Mkurugenzi wa chama cha waandishi wahabari wanawake Tanzania Znz Dk Mzuri Issa amesema watendaji wa Wizara husika kuepuka tabia ya usiri wa kutotoa taarifa muhimu zinazogusa maisha ya watu.

"Kuna usiri wa taarifa kwa baadhi ya watendaji hivyo tunaiomba Wizara ya Afya iendelee kutoa mashirikiano mazuri kwa waandhishi wahabari kwa sababu masuala ya kinchi nay a kijamii ni lazima yasikike kupitia vyombo vya habari," Dk Mzuri Issa, Mkurugenzi TAMWA,ZNZ.

Dk Mzuri amesema  masuàla yànayohusu nchi pàmoja na jamii lazima yasikike kupitia vyombo vya habari kwa wananchi kupaza sauti zao

"Ni haki ya kila mtu kupata taarifa na uhuru wa kujieleza na katiba zote mbili zimeeleza ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar na hata kidunia tumesaini mikataba  mbali mbali ya Kimataifa ikiwemo Africa Charter, Dk Mzuri Issa.

Mapema akiwasilisha ripoti hiyo Afisa Tathmini na Ufatiliaji Abdul Mohamed kutoka TAMWA ZNZ amesema ripoti hiyo imengunduwa mapungufu kadhaa kama vile ukusanyi wa takwimu zà uhakika pamoja na umri zinazohusu wanawake na wasichana zinazoonesha vifo wakati wa kujifunguwa.

“Baadhi ya mapungufu ni kutokuwepo takwimu sahihi za vifo na umri kwa wanawake na wasichana, tunaomba Wizara ya husika lifanyie kazi”, Abdul Mohamed.

Nae Afisa mradi wa kuendeleza utetezi kwa vyombo vya habari kwa wasichana na wanawake kutoka TÀMWA ZNZ Zaina Abdalla Mzee amesema lengo la mradi huo ni kuibuwa changamoto zinazowakuta kundi hilo pamoja na  vituo vya Afya na kuzitafutia ufumbuzi kwa wahusika.

"Tulianza kwa kufanya utafiti na kugunduwa waandishi wengi hawana uelewa juu ya masuala ya Afya ya uzazi hivyo tuliandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo na sasa wanaripoti vyema habari hizi na wanasaidia jamii kupata huduma stahiki,” Zaina Mzee.

Nao watendaji kutoka Wizara yà Afya Zanzibàr wamekiri kuwepo kwa baadhi ta changamoto katika sekta hiyo ikiwemo bajeti ndogo ukilinganisha na mahitaji ya wananchi.

Hata hivyo wàndishi wahabari waliopatiwa mafunzo kupitia mradi huo wamesema wanakabiliwa na changamoto wakati wa kuandaa habari pamoja na vipindi kwa bàadhi ya wandendaji wa Wizara hiyo kutotoa mashirikiano.

"Changamoto zinakuja kwa baadhi ya watendaji kutupiga danadana wakati wa kukusanya hizi taarifa kwa hivyo inatuwia vigumu kuzipata kwa muda sahihi na nyengine hazipatikani kabisa,” Waandishi wa habari.

Mradi wa kuendeleza utetezi wa haki ya elimu ya Afya ya uzazi kwa vyombo vya habari kwa wasichana na wanawake  unaotekelezwa na TAMWA ZNZ ulitowa mafunzo kwa waandishi wa habari 71 na wahariri 23 kwa Unguja na Pemba ambapo ulioanza October 2022 na kumalizika October 2023 ulitekelezwa kwa Wilaya ya Magharibi "B" na Kati kwa Unguja na Wilaya ya Chake Chake kwa Pemba.

Post a Comment

0 Comments