Ticker

6/recent/ticker-posts

Wakulima Wafunguka Mafanikio Waliyoyapata Kupitia Mradi Wa VIUNGO


NA AHMED ABDULLA, Zanzibar

Uwepo wa mradi wa viungo na mbogamboga umesaidia wananchi wengi kujishughulisha na kilimo hali iliyoleta mapinduzi ya kiuchumi katika familia zao.

Hayo yamebainishwa na wanufaika wa mradi huo mara baada ya kutembelewa na Kikosi Kazi cha ufundi kwa Taasisi zinazotekeleza mradi wa Kilimo cha Viungo, mboga mboga na matunda lengo likiwa ni kugunduwa Mafanikio ya mradi huo pamoja na changamoto zinazowakabili wakulima na kuzitafutia ufumbuzi.

Wamesena kuna mafanikio waliyoyapata kupitia kilimo ikiwemo kuimarisha Afya za familia kwa lishe bora kwa kula mboga mboga na kuongeza kipato kupitia mfumo wa biashara. 

Ali Shauri ni katibu wa uhirika wa kilimo hai kiitwacho TUMAINI LA KIJANI uliopo Chuini Zanzibar, amesema wao wanatengeneza bustani za nyumbani ambazo zinajumuisha mbogamgoga pamoja na mimea ya dawa lengo likiwa kukibadilisha kijiji cha kuwa kijiji cha kijani.

Amesema sababu zilizowapelekea kujiingiza katika kilimo hicho ni kuona jamii inakuwa na afya bora kwa kutumia vyakula wanavyovizalisha wenyewe kupitia kilimo hicho sambamba na kupunguza matumizi ya fedha.

“Sababu ambazo zimetufanya kuingia katika kilimo hichi ni kuzingatia suala ziama la afya bora kwa jamii kwa kutumia chakula walichokizalisha wenyewe ambacho ni salama ukizingatia kimezalishwa kwa kutumia teknolojia ya kilimo hai” amesema Ali Shauri

Amesema jamii ya kijiji hicho imeanza kuelewa dhamira ya kilimo hai katika kupunguza matumizi ya fedha na sasa wameondoa dhana ya kuliba bustani za maua na kuanza kulima bustani za mbogamboga.

“kabla hatujaanza mradi huu kulikuwa kuna watu wameweka bustani za maua lakini baada ya kuuelezea mradi huu katika kijiji chetu wenyi wamepunguza maua na kuanza kulima kilimo cha mbogamboga” Ameongezea

Akiyataja moja ya mafanikio waliyoyapata kupitia kilimo hicho amesema kwa sasa kumekuwa na uhakika ya upatikanaji wa chukula kwenye familia zinazojishughulisha na kilimo hicho.

“Familia zimeanza kuhakikisha upatikanaji wa chakula chao pamoja na kupunguza gharama za matumizi ya mbogamboga” Aliendelea kufafanua

Kwa upande wake Bi. Aviwe Ali Songoro ambaye anajishughulisha na kilimo cha Vanila, Migomba, Seshen na viungo vingine amesema awali alikuwa akijishughulisha na kilimo cha pilipili lakini mwanga kwake ulianza kung’aa baada ya kunufaika na mradi wa Viungo mboga na Matunda chini ya programu ya Agri-Connect.

“Nilianza kulima pilipili lakini baada ya kukutana na maafisa wa mradi wa viungo, mbogamboga na matunda wakanipatia mafunzo nilianza kujibadilisha na kuingia kwenye mazao mengine” Amesema Bi. Aviwe

Amesema alianza na ukulima wa vanila akiwa na mashina 200 ila uwezeshi wa mradio huo kwa kumpatia mbegu kwa sasa ana mashina 1,000 na tayar yameshaanza kutoa maua huku kwa upande wa migomba kwasasa anamiliki mashina 2,800.

“Nilianza na mashina 200 ya vanila ila mradi umeniwezesha na kwa sasa nina mashima 1,000 ambayo tayari imeshatoa Maua” Aliongezea 

Amesema amekuwa na mafanikio makubwa kupitia shughuli zake hizo za kilimo ambapo zinamsaidia kuendeshea maisha yake ikiwemo suala zima la mahitaji yake ya msingi pamoja na kuwasomesha watoto wake.

“Kwsasa nina uhakika wa mahitaji yangu na hivi sasa nawasomesha watoto wangu mmoja akiwa yupo chuo kikuu na namlipia kila kitu” Alisisitiza

Kama inavyofahamika kila penye mafanikio hapakosi changamoto ndio ilivyo pia kwa Bi. Aviwe ambapo yeye amesema uhaba wa maji wa kumwagilia mazao yake imekuwa ndioo kikwazo kikubwa kwake.

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji Mali Asili na Mifugo Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Pemba Muhandisi, Idriss Hassan Abdulla amepongeza juhudi zinazofanywa kwa pamoja na watekelezaji wa mradi wa viungo Zanzibar na ameahidi kuwa Wizara itaendelea kutoa mashirikiano ya kina ili kuona lengo la kuwawezesha wananche kwenye kilimo linafikiwa.

“Tumeona umuhimu wa sisi wizara kuwa na ushirikiano na washirika hawa wa miradi na tumejiridhisha kuwa ni kazi nzuri ambayo inalenga kutoa ajira pamoja na kuimarisha lishe bora kwa wananchi” Alisema Afisa huyo

Nae Meneja Mkuu wa Mradi wa Viungo Simon Makobe amesema wamefurahishwa kuona yale ambayo walikuwa wakiwafundisha wakulima hao wamekuwa wakiyazingatia na kuyafanyia kazi hali iliyoleta mabadiliko kutoka walipokuwa na walipo sasa.

“Tumefurahishwa kuona wakulima wameanza kuwa na mabadiliko kwenye utekelezaji wao mafanikio yameanza kuonekana” Amesema Simon Makobe

Vicent Akulumbuka kutoka timu wa washauri mradi wa VIUNGO kutoka Wizara ya Kilimo Tanzania, Dodoma amesema katika mradi huo wako katika hatua ya kujitathmini na kuangalia maendeleo ya mradi na changamoto zinazowkabili wakulima ili kuzipatia ufumbuzi.

“Tumeona wakulima wanajisaidia wenyewe kupata masoko lakini ikitokea kuna changamoto ya masoko sisi ndio kazi yetu kutatua changamoto hiyo” Amesem Akulumbuka

Ziara hiyo imejumuisha Ushirika wa kilimo cha bustani (TUMAINI LA KIJANI) kilichopo Chuini, Wilaya ya Magharibi “A”, Mkulima wa zao la Vanila Kizimbani na Kiwanda cha Uchakataji na usindikaji wa kiungo cha majani ya chai (ZANZIBAR ORGANIC INDUSRTY) kilichopo Amani viwanda vidogo vidogo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mradi hua wa Viugmgo unaotekelezwa kwa pamoja na TAMWA, People Developmend Forum (PDF) na Community Forest in Pemba (CFP) chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya.


    

Post a Comment

0 Comments