Ticker

6/recent/ticker-posts

Wenye Ulemavu Wapania Kuondosha Utegemezi

Mkufunzi wa mafunzo ya mbinu za kuanzisha na kuendesha biashara Muhidini Ramadhan Muhidini akieleza jambo katika mafunzo hayo kwa viongozi na wasimamizi  wa vikundi jumuishi vya wilaya ya Kusini Unguja yaliyofanyika katika ukumbi wa walimu Kitogani 

 

Na Ahmed Abdulla:

IKIWA imezoeleka kwa miaka ya hivi karibuni visiwani Zanzibar hasa kisiwa cha Unguja kuzuka tabia ya baadhi ya watu wenye ulemavu kukaa barabarani na wengine kutembezwa katika mitaa kwa ajili ya kuombaomba.

Jambo hili limeibua hisia za watu mbalimbali ikiwemo jumuiya zisizo za kiserikali kwa kuanza kulitafutia ufubuzi jambo hilo na kuwafanya watu wenye ulemavu kuwa na shughili za kujiingizia kipato na kuondokana na dhana hiyo.

Miongoni mwa jumuiya hizo ni chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Upande wa Zanzibar TAMWA-ZNZ ambapo wameshindikiana na shirikisho la jumuiya za watu wenye ulemavu zanziba SHIJUWAZA ambapo wanapigana kwa hali na mali ili kuona maisha ya watu wenye ulemavu si tegemezi.

Nairat Abdallah Ali ni Afisa uwezeshaji wanawake kiuchumi kutoka chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar amesema katika kuhakikisha wanafikia makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu wanatekeleza mradi jumuishi wa kuwawezesha watu wenye ulemavu kiuchumi (KIJALUBA Isave)

Amesema mradi huo wa miaka miwili una lengo la kuinua thamani ya watu wenye ulemavu kwa kuwawezesha watu wa jamii hiyo kiuchumi.

“lengo la mradi huu ni kuwafanya watu wenye ulemavu waweze kujitegemea kiuchumi,kuwa na shughuli za kufanya za kujiingizia kipatao pamoja na kuwa na akiha” amesema Afisa huyo

 

Amesema kupitia mradi huo huendesha mafunzo kwa watu wenye ulemavu yanayolenga kuwawezesha watu wenye ulemavu kufanya biashara ili kujikwamua kiuchumi kutokana na kundi hilo kuonekana lipo nyuma kimaendeleo.

Amesema mradi huo unatekelezwa kwatika wilaya mbili ambazo ni wilaya ya Kusini Unguja na Wilaya ya Chakechake Pemba na una jimla ya vikundi 43 na awamu ya kwanza waliwapa mafunzo ya kuweka na kukopa huku kwa awamu ya pili mafunzo yanawafundisha juu ya utambuzi na usimamizi wa biashara yaliyofanyika katika ukumbi wa walimu Kitogani wilaya ya Kusini Unguja.

“Awamu hii ni kubwa na muhimu kwani ili mtu aendelee kuweka akiba lazima awe na biashara ya kudumu” ameongeza

Kwa upande wao baadhi ya watu wenye ulemavu wilaya ya Kusini Unguja wamesema mafunzo ya mbinu za kufanya biashara yatawasaidia kuwaonesha njia za kuzifikia fursa za kujiingizia kipato na kujikwamua na umasikini unaoelekea kwenye utegemezi.

Mohammed Ali ni Mkaazi wa kijiji cha Paje yeye ana ulemavu wa uoni amesema awali alijuwa biashara ni kuuza na kuniniwa tu ila baada ya mafunzo hayo amejifunza ya kuchagua biashara,kupanga gharama,kupanga matumizi pamoja na masoko.

“natarajia kuanzisha biashara ambayo imezingatia vipengele vyote nilivyofundishwa na nina ibami itakuwa endelevu” amesema Mohammed

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mbinu za kuanzisha na kuendesha biashara wakisikiliza kwa umakini mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa walimu Kitogani ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa KIJALUBA iSAVE


Kwa upande wa Zawadi Ali Suleiman mkaazi wa Mzuri Makunduchi ambaye ana ulemavu wa viungo amesema kupitia mafunzo hayo yatamuwezesha kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa biashara zake ndogondogo.

“kwa sasa nafanya biashara zangu ndogondogo kama kuuza juisi na malai pamoja na kutekeleza kazi za shamani ila mafunzo haya yataleta mabadiliko kwangu na familia yangu” amesema mwanamama huyo

Mkufunzi wa mafunzo hayo Muhidini Ramadhan Muhidini ambaye ni afisa muwezeshaji wa masuala ya biashara na vikundi amewasisitiza wasimamizi hao wa vikundi wanapotaka kuanzisha biashara zao kuwa na malengo ikiwemo kujua faida , hasara na mitaji, soko na kudhibiti matumizi ya familia ili kuwa na biashara nendelevu.

Alisema vingi vingi havifikii malengo kutokana na kutokuwa na mipango Madhubuti ya kuendesha biashara zao.

“vikundi vingi vinakufa kwa kutokufuata utaratibu na miongozo ila kama utaifata miongozo hii biashara au kikundi kitadimu na kuwa na tija” amesema Mkufunzi huyo

Mafunzo hayo ya siku mbili kwa viongozi na wasimamizi wa vikundi jumuishi vya kuweka na kukopo wilaya ya kusini yameandaliwa na TAMWA Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa mradi huo.

Post a Comment

0 Comments