Na Theresia Severini:
Victory Wembanyama ni mchezaji wa
mpira wa kikapu wa San Antonio Spurs ya Chama cha Mpira wa Kikapu cha Taifa
(NBA) alizaliwa 4 Januari 2004 Le Chesnay nchini ufaransa.
Wembanyama alianza kazi yake mnamo mwaka 2019 na
Nanterre 92 ya LNB Pro A mnamo 2019. Miaka miwili baadaye, alihamia ASVEL na
kushinda taji la Pro A msimu wa 2022-23, baada ya hapo Wembanyama alisaini na
Metropolitans 92 na kuwa mchezaji mdogo zaidi kushinda tuzo ya Pro A MVP huku
akijipatia heshima za Pro A Best Defender na kuongoza ligi katika kufunga na
rebounds, Vilevile ametajwa kama LNB All-Star mara mbili, kushinda All-Star
Game MVP mara moja, na ni mchezaji bora wa Pro A mara tatu.
Waswahili wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka msemo
huu unajidhihirisha wa Victory Wembanyama kwa maana mcheza kikapu huyu anatokea
katika familia ya michezo kwani Mama yake ambaye ni Elodie De Fautereau alikuwa
ni mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu wa wanawake na kocha wa sasa wa mpira
wa kikapu wa vijana, Baba yake Felix Wembanyama aliwahi kujihusisha na mchezo
wa kuruka.
Itoshe kusema San Antoni Spurs haikukosea kumchagua Wembanyama kama chaguo loa la kwanza kati ya chaguo 30 za Raundi ya kwanza kwenye NBA Draft 2023. (NBA Draft Ni pale ambapo timu kutoka Chama cha Mpira wa Kikapu cha Taifa (NBA) huchagua wachezaji ambao hawajawahi kucheza katika NBA kabla).
Huyo ndio Victory Wembanyama mcheza kikapu mwenye urefu wa futi 7 inch 4 anaetajwa na ESPN kuwa maarufu zaidi ndani ya miezi 12 ijayo.
1 Comments
ahsanteni kwa taafifa
ReplyDelete