Ticker

6/recent/ticker-posts

Azam FC Yafurusha Watano Maandalizi Ya Msimu Mpya

 Ikiwa msimu wa 2022-23 umemalizika na Azam FC kutoambulia chochote ndani ya msimu mzima sasa klabu hiyo imeanza na uboreshaji wa kikosi chao kuanzia kwa wachezaji na Benchi la ufundi.

Katika maboresho hayo ni kuanza kuondoa wale ambao hawana mahitaji nao katika msimu ujao ambapo leo wameanza na kuondoa viongozi wawili wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji watatu.

Waliachwa kwenye benchi la ufundi ni Kocha wa Magolikipa raia wa Uhispania Daniel Caden na Kocha wa Viungo Dkt. Moadh Hiraou huku taarifa ya klabu hiyo ikieleza ni makubaliano ya pande zote mbili.

Upaande wa wachezaji waliochwa ni pamoja na beki kisiki Bruce Kangwa aliyehudumu klabuni hapo kwa miaka saba ya nguvu, tokea aliposajiliwa mwaka 2016 ukitoka Highlanders FC ya Zimbabwe.

Wachezaji wengine waliopewa mkono wa kwaheri ni mshambuliaji Rodgers Kola raia wa Zambia, na kiungo Kenneth Muguna raia wa Kenya.

Ikumbukwe ni karibia wiki moja tangu klabu hiyo imtambulishe kiungo mzanzibar Feisal Salum Abdalla aliyetokea Yanga ambaye atahudumu klabuni hapo kwa mkataba wa miaka mitatu.


Post a Comment

0 Comments