Ticker

6/recent/ticker-posts

Wadau wa sekta ya habari Z’bar wataka ushirikishwaji zaidi utungwaji wa Sheria

 

Mwandishi wa habari mwandamizi Zanzibar Salim Said Salim akichangia katika mkutano uliofanyika ofisi za TAMWA-ZNZ Tunguu Wilaya ya kati Unguja. Picha na Muhammed Khamis 


Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wahabari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt Mzuri Issa amesema kuna haja ya ushirikishwaji kikamilifu kwa waandishi wa habari katika michakato ya uundwaji ama urekebishwaji wa sheria mbali mbali zinazohusu umma.

 

Dkt Mzuri ameyasema hayo katika ukumbi wa Chama hicho Tunguu Wilaya ya kati mkoa wa kusini Unguja alipokua akizungumza na wadau kutoka taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi katika mkutano wa siku moja uliokua na lengo la kuzitazama na kutoa maoni yao kwa baadhi ya sheria ikiwemo sheria ya tume ya uchaguzi,sheria ya habari na sheria ya takwimu Zanzibar.

 

Alisema kuna baadhi ya sheria zinazonekana kuleta mkanganyika katika utekelezaji wake huku baadhi ya sheria hizo zikionekana kuminya uhuru wa habari na waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa maslahi ya Umma.

 

‘’Ili kuepuka haya ni vyema sisi waandishi wa habari tukashirikishwa kikamilifu tangu hatua za awali kwenye uundwaji wa sheria ili kutoa maoni yetu pale tunapoona hapatakua sawa hususani katika utendaji wetu wa kazi’’aliongezea.

 

Kwa upande wake mwanahabari  mwandamizi Zanzibar Salim Said Salim alisema kuna baadhi ya sheria ni za ajabu sana akitolea mfano kipengele cha sheria ya uchaguzi kinachomkataza mwandishi wa habari kutojumuisha matukio ya uchaguzi yaliobandikwa vitu vya kupigia kura na maafisa wenyewe wa tume hiyo.

 

Alisema kipengele hicho cha sheria kinakiuka sana uhuru wa habari na kueleza kuwa kuna haja ya kufanyiwa marekebisho haraka sana ili waandishi wa habari waweze kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

‘’Kwa kuwa maafisa wenyewe wa tume ya uchaguzi ndio waliojumuisha na kubandika matukio ya kura kwenye vituo vya kupigia kura huku karatasi hizo zikiwa tayari zimetiwa saini za wahusika kwanini mwaandishi wa habari azuiwe keshiria kutojumuisha idadi ya kura husika kutoka kwenye vituo’’alihoji mwanahabari huyo.

 

Akichangia katika mkutano huo mwandishi wa habari kutoka shirika la magazeti ya Serikali Tanzania Bara (TSN) Issa Yussuf alisema ili kuna haja kubwa ya wanaohusika na undwaji na urekebishwaji wa sheria kuratibu mpango mzima wa kukusanya maoni ya watu kabla ya kutengeneza sheria ukizingatia wao ndio walengwa wakubwa wa sheria zinazotungwa hivyo ni wajibu kutoa maoni yao na kuzingatiwa.

 

Mratib wa Baraza la habari Tanzania MCT Shifa Said Hassan alisema uwepo wa sheria bora katika Nchi na umuhimu wa kufuata mikata ya kimataifa ni jambo la msingi na linalopaswa kutiliwa mkazo zaidi na kila mmoja.

 

Mkutano huu wa siku moja umeitishwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Internews Tanzania uliokua na lengo la kupitia baadhi ya sheria Zanzibar na kutoa maoni yao  juu ya yaleo wanayoona yanahitaji kufanyiwa marekebisho.

Post a Comment

0 Comments