Mkurugenzi wa uchaguzi Khamis Kona Khamis akiwa pamoja na Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa mara baada ya kumaliza mkutano wa majadiliano katika ofisi za Tume hiyo Maisara mjini Unguja, |
Na Ahmed Abdulla
Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA-ZNZ kimesema
wakati umefika kwa Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuhakikisha kinaweka
mazingira ya usawa wa kijinsia katika utekelezaji wa shughuli zao mbali mbali
zikiwemo za usimamizi wa chaguzi na nyenginezo.
Kauli hiyo imekuja kufuatia mkutano malumu wa
majadiliano baada ya kumalizika kwa mkutano awali uliofanyika mwezi
septemba mwaka jana na kupeana na majukumu kwa pande zote mbili kupitia
sera jinsia ya mjumuisho kwa ajili ya kutazama uwepo wa mazingira ya
usawa wa kijinsia katika muundo wa tume hiyo na utendaji wa kazi zake.
Akizunguma katika mkutano huo Mkurugenzi wa Chama hicho
Dkt,Mzuri alisema ushiriki wa wanawake katika shuhuli za tume hiyo utaleta
mwanga zaidi na hatikame kuwafanya wanawake wengi waweze kufikia malengo yao
yakiwemo ya kuwa viongozi.
Alisema kwa miaka mingi katika kazi za tume hiyo kumeonekana
wanaume wengi ndio wanaoshiriki shughuli za tume zikiwemo za usimamizi wa
chaguzi zinazofanyika huku idadi kubwa ya ushiriki ikionekana kuwa ya wanaume
na wanawake kuwa nyuma licha ya kuwa ndio wenye idadi kubwa katika kila chaguzi
zinazofanyika.
Alisema iwapo wanawake wengi watashiriki katika utendaji wa tume
hiyo utapelekea wanawake wengi zaidi kushiriki katika harakati za kuchagua na
kuchaguliwa na hatimae idadi kubwa ya wanawake kutumiza ndoto zao za kuw
aviongozi itafakiwa.
‘’Hata kama ikitokea idadi kubwa ya wanawake hawakuomba nafasi
kwenye tume lakini muna wajibu wa kukweka kanuni ambazo zitalazimisha asasi za
kiraia kupeleka idadi kubwa ya wanawake katika shughuli za tume zikiwemo zile
za usimamizi wa chaguzi zinazofanyika kila baada ya miaka mitano’’aliongezea
Dkt,Mzuri.
Kwa upande wake mkuu wa miradi TAMWA-ZNZ Ali Mohamed alisema wakati mabadiliko hayo ya kuleta usawa wa kijinsia yanaendelea kufanyika kunahitajika kujengwa mazingira lazimisha katika sheria ya msajili wa vyama vya siasa ambayo itaonesha uwepo wa idadi sawa ya ushiriki wa wanawake katika kugombe anafasi za uongozi.
Alisema kuwepo kwa sheria hiyo kutapalekea mazingira rafiki kwa wanawake wengi na kuondoa ukandamizwaji ambao kwa miaka mingi wanawake wamekua wakilalamika, na wanadai kuwa hufanywa na watu wenye nafasi za maamuzi kwenye vyama vyao kupitia idadi kubwa ya wagiombea kuwa wanaume na wananwake huwa wachache.
Awali Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Khamis Kona Khamis alisema mkutano huo wa majadiliano umekuja wakati muafaka ambapo tume hiyo ipo kwenye mchakato wa kulifganyika kazi suala hilo.
Smbamba na hayo alisema licha ya uwepo wa changamoto za hapa na pale lakini kwa kiasi kikubwa tume hiyo inaendelea kufanyika kazi maswala ya kijinsia na ndio maana baadhi ya wilaya zikiwemo kaskazini Unguja maafisa wote wa tume hiyo ni wanawake.
Pamoja na hayo alisema
bado TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na asasi nyengine za kiraia wana wajibu wa
kupeleka mapendekezo yao pale wanapoona kuna changangamoto za mifumo na iwapo
watafanya hivyo watasaidia sana utendaji kazi wa tume hiyo na kupeleka mbele
maendeleo kwa maslahi ya Taifa.
0 Comments