Ticker

6/recent/ticker-posts

Mkurugenzi ZEC akaribisha wadau kuongeza idadi ya wanawake katika uongozi

Mkurugenzi wa Uchaguzi ZEC Khamis Kona Khamis alipokua akizikiliza michango ya wajumbe wa mkutano huo.


Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khamis Kona Khamis amesema tume hiyo ipo tayari kufanya kazi na TAMWA-ZNZ katika kuwaendeleza wanawake wengi zaidi kushika nafasi za auongozi. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume hiyo Khamis Kona Khamis wakati wa mkutano wa majadiliano uliotazama ushiriki wa nafasi za wanawake katika shughuli mbali mbali za tume hiyo.

 Alisema kwa kiasi kikubwa uwepo wa TAMWA-ZNZ na asasi nyengine unasaidia kupaza sauti za wanawake wengi na kuna kila sabababu ya kutolewa kwa mashirikiano zaidi ili kutimiza dhamira hiyo.

 Awali alisema wao kama tume wanafanya jitihada kubwa kuhakikisha wanawake wanahika nafasi na ndio maana zipo baadhi ya wilaya mafias wa tume hiyo wote ni wanawake.

 Akichangia mkutano huo Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa alisema iwapo kutakua na mazingira bora na rafiki katika utendaji kazi wa tume hiyo na kushirikisha wanawake wengi zaidi itasaidia kuongeza idadi kubwa ya wanawake kushika nafasi za uongozi.

 Alisema wanawake wengi wanashindwa kutimiza malengo yao kutokana na kukosekana kwa msingi imara ambao ulipaswa kuonekana awali kwenye tume hiyo.

Post a Comment

0 Comments