Ticker

6/recent/ticker-posts

Zanzibar University Yaweka Kambi Kuwasaidia Wanafunzi Wanaotaka Kujiunga Elimu Ya Juu

 


Wanafunzi wenye lengo la kujiunga na vyuo vya elimu ya juu wameshauriwa kutafuta ushauri kutoka kwa wataalamu ili kusoma kada wanayoihitaji.

Ushauri huo ulitolewa na Msaidizi mkufunzi kutoka chuo cha Zanzibar University Nassra Nassor Suleiman, katika maonyesho maalumu ya chuo hicho yenye lengo la kuwapatia ushauri wanafunzi wanaohitaji kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kujuwa namna ya ufaulu wao  unavyowaweza kujiunga na kada kulingana na ufaulu huo yanayoendelea katika viwanja vya mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi, Kisonge.

“Wanafunzi wanashindwa kutambua kada wanazoweza kusoma kulingana na ufaulu wao” Alisema Bi, Nassra

Aidha alisema wanafunzi wengi hupata alama zinazowawezesha kusoma kada zinazohusisha masomo ya sayansi lakini wanashindwa kutambua hilo na badala yake hujiunga na kada ambazo hawakuzihitaji.

Sambamba na hayo amewaomba wanafuzi kufika katika maonyesho hayo ili kupata ushauri huo pamoja na kupata usajili wa kujiunga na chuo hicho unataotolewa hapo hapo.

“Tunawaomba wanafunzi wajitokeze hapa kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge ili wapate ushauri na Kujisajili kwa lengo la kujiunga na chuo chetu” Aliongezea Bi. Nassra

Kwa upande wake mratibu wa astashahada na stashahada kutoka chuo hicho Hamed M. Salum amesema miongoni mwa huduma nyingine zinazopatikana katika maonyesho hayo ni kuombewa namba ya utambulisho wa stashahada (AVN) pamoja na kufahamishwa kujiunga na kozi za msingi kwa wale ambao ufaulu wao hauruhusu kujiunga na chuo moja kwa moja Ambazo zinatolewa na Open University.

Post a Comment

0 Comments