Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema ili tuweze kukuza usawa wa kijinsia visiwani Zanzibar kuna ulazima waandishi wa habari kutoa taarifa za wanawake na maendeleo yao katika Nyanja tofauti zikiwemo za uongozi, na maendeleo ya kijamii.
Amesema ili usawa wa kijinsia upatikae ni lazima kuwe na mkakati maalumu wa kuwajenga waandishi wa habari chipukizi ambao wataweza kutoa habari zinazohusus wanawake kwa ufanisi mkubwa.
Aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa siku moja wa kupitia mtaala maalumu utakaotumika kufundishia waandishi wa habari vijana kupitia mradi wa kuwajengea uwezo wanawake na uongozi kupitia vyombo vya habari.
‘’Kwa kuwa wanahabari ni sauti ya wasio na sauti, kuwa kupitia mafunzo hayo maalumu yatakayowajengea uwezo wanahabari vijana 18 kutoka Unguja na Pemba ninaamini kwamba watakwenda kutatua tatizo la muda mrefu lililokosa wakulisemea na kuwafanya wanawake wengi zaidi kushindwa kufikia malengo yao’’aliongezea.
Sambamba na hayo alisema pia mafunzo
hayo yatawajenga wanahabari waweze
kuandika habari zenye kuleta manufaa zaidi sambaba na kuwa wachambuzi wa mambo
mbali mbali kupitia maandiko yao au vipindi watakayotaarisha wakati wakiendelea
na mafunzo yao ya mwaka mmoja.
Awali akiwasilisha ripoti ya mtaala
utakaotumika kuwafundishia wanahabari hao vijana Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha
Taifa Zanzibar Dkt,Salum Sleiman Ali alisema wakati TAMWA-ZNZ inajipanga
kufanya mafunzo kwa wanahabari hao vijana hawana budi kuzingatia yale yote
yalio muhimu ambayo wanaamini yatawajengea uwezo wanahabari hao na kuwafanya
kuwa wadadisi.
Baadhi ya wajumbe wakichangia ripoti
hiyo walisema ni jambo jema kuwajengea uwezo wanahabari na walisema ni wajibu
wa wale wote ambao watanufaika na mafunzo hayo kufanya kazi kwa bidii kuonesha
uwezo wao wa kuisaidia jamii ya wanawake.
Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Taifa
Idara ya habari Imane Duwe alisema
katika mafunzo hayo wanahabari wanapaswa pia kufundishwa namna bora ya
kujitegemea na kujitolea zaidi kutokana
na kuongezeka kwa wimbi kubwa la changamoto katika upatikanaji wa ajira.
Mradi wa kuwakuwaza wanawake katika katika nyanja mbali mbali za kijamii kupitia vyombo vya habari utawashirikisha wanahabari vijana vijana 18 Zanzibar, unatekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na shirika la The National Endowment for Democracy (NED) kutoka
Marekani.
Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akizungumza na wajumbe wa mkutano huo wa siku moja katika ofisi za Chama hicho Tunguu Wilaya ya kati Unguja. |
Picha ya pamoja kwa washiriki wa mkutano huo mara baada ya kumaliza kuwasilishwa kwa ripoti hiyo. |
Baadhi ya maafisa wa
TAMWA-ZNZ wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa ripoti hiyo. |
0 Comments