Ticker

6/recent/ticker-posts

Uhuru wa kujieleza unavyoweza kuchangia ukuaji wa kasi ya maendeleo

 




Na Ahmed Abdalla

Kwa miaka mingi watalamu na wadadisi mbali mbali ulimwemguni kote wamediriki kusema hakuna jamii yoyote hile inayoweza kupiga hatua kimaendeleo iwapo wananchi wake hawatakua na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yao.

Kwa minajili hii tunaaminishwa na kuamini kuwa uhuru wa kujieleza ni nguzo muhimu ya kusukuma maendeleo mdami ya Nchi yoyoter hile.

Visiwani Zanzibar inaendelea kuaminika kuwa hadi sasa bado haki hii ya kujieleza imekua ikakandamizwa kwa kiasi Fulani kupitia sharia ya habari ya mwaka 1988.

Licha ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania na hile ya Zanzibar kuweka wazi haki hio ya kujieleza lakini bado sharia nyengine zimekua zikikandamiza na ndio maana wadau wa habari visiwani hapa wanaeleza kuwa haki hiyo imetolewa kwa mkono wa kulia na kunyanganywa kwa mkono wa kushoto.

Kutokana na uwepo wa mazingira hayo Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Internews Tanzania wanaendelea na mradi maalumu wa kuwakutanisha wanahabari kutazama na kujadili kwa pamoja sharia hiyo ya habari na kasha kutoa mapendekezo yao ili yaingizwe kwenye sharia mpya ya habari inayosubiriwa kwa hamu visiwani hapa.

Wakiwa katika majadiliano ya kupitia sharia hiyo baadhi ya waandishi wa habari visiwani hapa walionesha miongoni mwa sehemu ambazo wanaamini kuwa zinanyima uhuru wa kujieleza sambmba na uhuru wa habari kiujumla.

Kwa mfano moja miongoni mwa vipengele vya sharia hiyo kinasema Kifungu cha 27 (2) Hakimu yeyote anaweza kutoa hati kumuidhinisha afisa polisi yeyote wa cheo cha Inspekta, kwa msaada au bila msaada kuingia na kupekua mahali popote pale ambapo inashukiwa kuwa kuna gazeti linachapishwa kinyume na Sheria hii linafanya kosa  chini ya Sheria hii au kanuni zozote zilizotungwa ama limefanya, linafanya au linakaribia kufanya kosa, hivyo anaweza kukamata.

Miongoni mwa washiriki walisema kitendo cha sharia hiyo kulipa mamlaka makubwa jeshi la polisi ni kukandamiza uhuru wa habari na uhuru binafsi wa mtu kujieleza na sharia hiyo inapaswa kubadilishwa ili kuendana na wakati tuliona.

Juma Khamis alisema anaamini iwapo mazingira bora na sharia imara itakapokamilika Zanzibar itapiga hatua kubwa zaidi za kimaendeleo na kuwa mfano duniani kote.

Issa Yussuf alisema licha ya uwepo wa changamoto hizo lakini kuna haja ya wanahabari kutambua sharia wanazozifanyia kazi kila leo ili kujiweka katika mazingira salama muda wote.

Awali mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa alisema wanahabari wanawajibu mkubwa kuhakikisha Zanzibar inapata sharia bora ya habari kwa maslahi mapana ya tasnia na Taifa kwa ujumla.

Alisema sharia iliopo sasa ya habari haiendani na wakati tulionao na hwenda ilitungwa katika kipindi ambacho wengi waliokua hawajaona umuhimu wa mambo mengi ambayo sasa yamejitokeza hivyo kuendelea kuyawekea sharia ngumu ni kunyima uhuru wa walio wengi ambao nao pia wanapaswa kusikilizwa.

 

 


Post a Comment

0 Comments