Klabu ya Azam FC imeingia mkataba wa miaka miwili na golikipa, Ahmed Ali Suleiman 'Salula', akitokea KMKM ya Zanzibar.
Taarifa
iliyochapishwa leo August 3, 2021 katika ukurasa wa instagram ya klabu hiyo ikimuonyesha
mtendaji wa klabu hiyo Abdulkarim Amin ‘Popat’ na Salulu wakisaini kwenye
mkataba huo huku kukiwa hakujaainishwa
thamani ya mkataba huo.
Salula alitamba katika mashindano
Cecafa Senior challenge ya mwaka 2017 akiwa na timu ya taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' wakimaliza
mashindano hayo wakiwa makamu bingwa hivyo usajili wake ndani ya klabu hiyo ni
kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ndani ya klabu ya Azam FC.
Huo unakuwa usajili wa saba kwa klabu hiyo ikiwa ni kujiandaa na msimu ujao, huku nia ya klabu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC).
0 Comments