Ticker

6/recent/ticker-posts

"TUWAKATAE WENYE LENGO LA KUTUGAWA" MAALIM SEIF


 

Makamu wa kwanza wa rais wa zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar haitomvumilia mtu yeyote ambaye ataleta uchochezi wa kuwagawa wananchi na kuanzisha hasama miongoni mwao.

Amewataka wananchi Kudumisha Amani Na Umoja uliopo na kukataa vitendo vya wale wanaopinga umoja uliopo Nchini kwani kufanya hivyo kutapelekea kuipatia Zanzibar Maendeleo kwa haraka.

Maalim Seif aliyasema hayo alipojumuika na Waumini Wa Dini Ya Kiislam katika Ibada Ya Sala ya Ijumaa Katika Msikiti Wa Ar Rahma Uliyopo Bububu Kijichi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Maalim seif ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha  ACT wazalendo alisema wako watu ambao hawaridhishwi na mshikamano unaofanywa na wanachi jambo ambalo linaweza kuzorotesha ukuwaji wa maendeleo katika taifa.

Alisema kuwa kuwepo kwa umoja na mashirikiano ya wananchi ni jambo la muhimu katika nchi na kuwataka watu waachane na ubaguzi kwa kuangalia itikadi za kisiasa katika masuala ya kusimamia maendeleo yao.

“Kama tukiwa wamoja ni rahisi nchi yetu kupiga hatua za kimaendeleo katika Nyanja zote na kuwa mfano wa nchi nyingi za Afrika” alieleza Maalim Seif.

Sambamba na hilo Makamu wa Kwanza wa Rais aliwataka wananchi kuacha ubaguzi wa rangi au wa kisiasa kwani mbora kwa mwenyezi ni Yule mchaji zaidi.

Maalim Seif alisema dhamira ya yeye na Rais wa Zanzibar Dr. Husein Ali Hassan Mwinyi ni kufanya kazi kwa pamoja ni kuondoa changamoto ambazo hupelekea wananchi kutofautiana na kuleta chuki miongoni mwao.

“Tumeunda serikali hii ya shirikishi ili hasama na chuki zoote zinazosababishwa na uchaguzi zisijirudie tena kwani hazi tija wananchi wetu” alieleza maalim Seif.

Alisema kuwa wazanzibar watakuwa wamoja vitendo vyoote viovu vitakuwa historia pamoja na vurugu zinazotokea katika kipindi cha uchaguzi.

Alisema kuwepo kwa Serikali yenye muundo wa umoja wa kitaifa ni njia moja ya kubaini sababu ya kupata dawa kulinda Zanzibar isirejee tena katika migogoro isio yan lazima.

Maalim Seif alisema wazanzibar wamebahatika pia kupata dini ya Kislamu ambayo katika maeneo mengi inasisitiza umoja miongoni mwa  jamii ya Waslamu kwa wazanzibar asiliimia kubwa ni waumini wa dini hiyo.

“Tumuombe mwenyezi Mungu atulinde na maaduwi ambao hawapendi umoja wetu” alieleza Maalim Seif.

 

Post a Comment

0 Comments