Ticker

6/recent/ticker-posts

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 06.12.2020 ZIKIMUHUSISHA FERNANDES, LINGARD, LUKAKU, BALOTELLI, STONES, MBAPPEPAMOJA NA TOSUN

 

Inter Milan itaanza mazungumzo na aliyekuwa mshammbuliaji wa Everton na Manchester United Romelu Lukaku juu ya mkataba mpya huku timu kadhaa zikimnyatia mshambuliaji huo wa Ubelgiji ikiwemo Juventus. (90 Min)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool na Manchester City Mario Balotelli yuko tayari kusaini mkataba na klabu ya Serie B ya AC Monza katika makubaliano ya hadi mwisho wa msimu. Mchezaji huyo, 30, amekuwa bila klabu tangu alipoondoka Brescia timu hiyo iliposhushwa daraja msimu uliopita. (Sky Sports)

 

Manchester United iko tayari kumzawadi kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 26, mkataba mpya ambao mshahara wake utaongezwa mara mbili na kufikia kima cha pauni 200,000 kwa wiki na kumaliza jitihada za Barcelona na Real Madrid waliokuwa pia wanamkodolea macho. (Sunday Mirror)

 

Timu kadhaa za Ligi ya Premier na Scotland zinamnyemelea Jesse Lingard

Kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 27, yuko tayari kuiomba Manchester United imruhusu kuondoka Januari, huku klabu kadhaa za Ligi ya Premier na zile za Scotland za Rangers na Celtic zikisemekana kuonesha nia ya kutaka kumsajili. (Team Talk)

Hata hivyo, Manchester United iko tayari kuongeza mkataba wa Lingard kwa mwaka mmoja zaidi - licha ya kuendelea kukosekana katika timu ya kwanza. (Star on Sunday)

 

Mlinzi John Stones akipasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mchuano

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ameitaka iliyokuwa klabu yake Manchester City kuendelea kumfahamisha kuhusu upatikanaji wa mlinzi wa England John Stones, 26. (90 Min)

 

 

Mkurugenzi wa Paris St-Germain Leonardo anasema klabu hio inapiga hatua wakati inapoendelea kutafuta mbinu za kumshikilia mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21. (Goal)

 

Jose Mourinho anasema Tottenham "haikupoteza muda wetu" kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Willian, 32, kwasababu hawakuweza kufikia ofa ya Arsenal. (London Evening Standard)

 

Leicester City imehusishwa na winga wa Sporting Lisbon raia wa Ecuador Gonzalo Plata, 20. (Vitotvo, via Leicester Mercury)

 

 

 

 

Aliyekuwa mlinzi wa Liverpool Conor Coady, 27, beki wa kati wa Wolves na England, alijua kuwa aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Molineux na mshambuliaji wa Ureno Diogo Jota, 24, ataonesha matokeo chanya haraka mno Anfield. (Liverpool Echo)

Na mechi ya Newcastle dhidi ya West Brom Jumamposi ijayo ipo "mikoni mwa wahudumu wa afya", kulingana na kocha wa Baggies Slaven Bilic. (Newcastle Chronicle)

 

Na haimae Rais wa Besiktas Ahmet Nur Cebi amekubali kufuatilia kwa karibu kumsajili tena mshambuliaji wa Everton raia wa Uturuki Cenk Tosun, 29, lakini amedokeza kuwa upande wake unaweza tu kufikia makubaliano ya mkopo. (Liverpool Echo)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amewasiliana na kiungo wa kati wa RB Salzburg raia wa Hungary Dominik Szoboszlai, 20, akiwa na matumaini ya kumshawishi akubali usajili wa klabu hiyo ya Uhispani. (Bild, via AS)

Timu ya Serie A ya Bologna inamnyatia mshambuliaji wa Wolves Patrick Cutrone, 22, raia wa Italia ambaye sasa hivi yuko kwa mkopo Fiorentina. (Il Resto del Carlino, via Sport Witness)

 

 CHANZO: BBC

Post a Comment

0 Comments