NA SITI ALI,ZANZIBAR
WADAU wa vyombo vya habari wameiomba
serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kukamilisha mchakato wa marekebisho ya sheria
za habari zilizotolewa maoni na wadau ili
kutoa mazingira rafiki kwa waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao
bila vikwazo.
Kwani ni muda mrefu sasa licha ya wadau
mbalimbali kutoa na kuwasilisha mapendekezo yao kuhusu mapungufu yaliyopo
kwenye baadhi ya sheria hizo, lakini utekelezaji wake bado umekuwa wa kusuasua
jambo linalopelekea mazingira magumu ya utendaji kazi wa vyombo vya habari
nchini.
Wadau wa
habari wamefanya mapitio ya sheria nane za habari ikiwemo Sheria ya usajili wa
wakala wa habari, magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa
marekebisho na sheria no.8 ya 1997, Sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar namba
7 ya mwaka 1997 iliyorekebishwa na
sheria namba 1 ya mwaka 2010 na kuwasilisha ripoti ya mapendekezo yao kwa
mamlaka husika ikiwemo kukutana na Rais na waziri.
Afisa program
wa masuala ya utetezi na uchechemuzi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania (TAMWA –ZNZ) Zaina Abdallah Mzee amesema kuwa wanachukuwa jitihada
mbali mbali za kuzisemea sheria zote zinazohusu habari ambazo haziko huru na
rafiki kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari ambazo ni sheria ya Wakala wa Habari Vitabu
na Magazeti ya mwaka 1988,sheria ya Tume ya Utangazaji,sheria ya Uchaguzi na
nyenginezo ambapo sheria zote hizi zinawakwaza waandishi wa habari na vyombo
vya habari na badala yake kupendekeza kuwekwa sheria moja tu ambayo ni rafiki
kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari katika kazi zao.
“Tumekuwa
tukipaza sauti zetu kwa muda mrefu sasa kupatikana sheria mpya ya habari
Zanzibar kuzisemea sheria ambazo zinawakwaza na zina mapungufu kwa waandishi wa
habari na badala yake kupendekeza sheria moja tu ambayo ni rafiki kwa waandishi
wa habari”anaeleza Zaina.
Aidha Zaina
ameelezea mashirikiano yao baina ya Jumuiya waandishi wa habari na maendeleo
Zanzibar ( ZAMECO) na Serekali Ikiwa ni pamoja na kukutana na kufanya
mazungumzo viongozi wa nchi akiwemo Rais na Waziri wa habari ,Tume ya
kurekebisha sheria ,Idara ya habari maelezo, wajumbe wa baraza la wawakilishi
ambapo wote hawa wamekiri kuwepo kwa mapungufu katika sheria ya habari iliyopo.
“Mashirikiano
ni mazuri baina yetu na Serekali kwani tumepata kufanya mazungumzo na viongozi
mbali mbali wa nchi akiwemo Waziri wa
habari,Tume ya Utangazaji,Tume ya kurekebisha sheria,Idara ya habari
maelezo,wajumbe wa baraza la wawakilishi na kukiri kuwepo kwa mapungufu katika
sheria ya habari iliyopo na kuwahidi kufanyia marekebisho na badala yake
kupendekeza kuwepo kwa sheria moja tu itakayokidhi vigezo vya habari”ameeleza Zaina.
Hata hivyo
ameelezea mikakati waliyojiwekea katika kupaza sauti juu ya mapungufu yaliyomo
katika sheria iliyopo na kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wachanga
kuripoti masuala ya sheria yahabari iliyopo, kupigania kuwekwa kwa sheria mpya
ya habari ambayo ni rafiki kwa waandishi wa habari sambamba na kutoa wito kwa
Serikali na wadau wa habari(watunga sera)kufanya hima suala la sheria mpya ya
habari kwani sheria iliyopo sio rafiki
kwa waandhishi wa habari na vyombo vya habari.
“ Wito kwa
Serekali na wadau wa habari pamoja na watunga sera na sheria kufanya hima suala
la sheria mpya ya habari kwani ni kilio kwa waandishi wa habari ambapo sharia
iliyopo sio rafiki kwa waandhishi wa
habari na vyombo vya habari kwani kufanya hivyo kutapelekea kupata maendeleo
katikakwani mwandishi wa habari ni sauti ya wasio na sauti “amesema Zaina.
Akifafanua
kuhusu maendeleo ya mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari Zanzibar,
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar ,Salum Ramadhan Abdallah
alieleza kuwa sheria ya habari ipo tayari kufanyiwa marekebisho kwani tayari
mapendekezo ya sheria hizo zipo katika hatua nzuri kwani imeanza kuchukuliwa
maoni.
Wadau mbali mbali,hivyo atahakikisha sheria hii
ataisimamia hadi kupitishwa,kwani ni ya muda mrefu sasa tokea kutolewa
maoni, ulipoanza mchakato wa sharia mpya
,hivyo ameahidi kufika mwisho wa suala
hili hivi karibuni.na kuwatoa hofu wanahabari juu ya suala zima la kupata
sharia mpya ya habari.
"Kwa
sasa sheria ya habari ipo tayari
kufanyiwa marekebisho kufanyiwa marekebisho kwani tayari mapendekezo ya sheria
hizo zipo katika hatua nzuri kwani imeanza kuchukuliwa maoni na wadau mbali
mbali,hivyo nitahakikisha sheria hii kuisimamia hadi kupitishwa,kwani ni ya
muda mrefu sasa tokea kutolewa maoni,hivyo ameahidi kulifikisha mwisho suala hili la sheria mpya hivi
karibuni,
Nawatoa hofu
wanahabari juu ya suala zima la kupata sheria mpya ya habari ambayo itakwenda
sambamba na misingi ya vyombo vya habari pamoja na wanahabari kwa ujumla”alieleza
Salum.
Aidha Salum
alisema tayari serikali imekamilisha mchakato wa kuandaa Sera mpya ya habari
Zanzibar na kuwatoa hofu wadau wa habari juu ya uwepo wa sera hiyo kuwa
itazinduliwa muda sio mrefu.
Mwandishi wa
habari mkongwe Salim Said alieleza kuwa
uwepo wa sheria bora ni muhimu katika kuwezesha mazingira bora ya waandishi wa
habari na kuwajibika kwani uhuru wa
habari na haki ya kujieleza ni nguzo muhimu za utawala bora kwasababu
inapelekea umma kuelea vyema kinachoendelea kati yao na kusaidia uwajibikaji na
unakuza mjadala na maarifa juu ya masuala mbali mbali.
"Vyombo
vya habari ni washirika wa maendeleo, kuwa na sera na sheria bora iliyo rafiki itawawezesha
waandishi wa habari kuwa na mazingira mazuri na rafiki katika
kutekeleza majukumu yao, kwani uhuru wa habari na haki ya kujieleza ni
nguzo muhimu za utawala bora kwasababu inapelekea umma kuelewa vyema
kinachoendelea kati yao, na kusaidia uwajibikaji na unakuza mjadala na maarifa
juu ya masuala mbali mbali katka nchi" alifahamisha, mwandishi wa habari
huyo mkongwe Zanzibar.
Mwandishi wa
Habari kutoka Gazeti la Chanzo Najjat Omar anasema sheria za habari zikifanyiwa
mabadiliko kutaongeza uwajibikaji kwa watendaji kwa sababu sharia zilizopo
zinawabana sana waandishi wa habari na kupelekea kukosa kufanya kazi kwa woga
Zaidi,hali inayopelekea mamlaka kukosa uwajibikaji.
“Matarajio
yangu ni kuiona serikali inabadilisha sheria kandamizi na ngumu kwa waandishi
wa habari ambazo zinarejesha nyuma sekta ya habari na badala yake kuweka sheria
mpya zilizo rafika kwa waandishi ambazo zitapelekea kutekeleza majukumu yetu kwa
ufanisi zaidi”anaeleza Najjat
Mwanasheria
wa kujitegemea ndugu Muhammed Faki Khatib amesema kuwa kutokuwepo kwa sheria
rafiki za habari kwa waandishi wa habari kutapelekea kukosa mabadiliko nchi
hasa katika tasnia ya habari pamoja na kukosa maendeleo kwani sheria zilizopo
hazina uhuru kwa waandishi na kupelekea kukosa uwajibikaji katika majukumu yao.
Hii inatokana
na kuwepo kwa sheria ambazo hazitowi uhuru kwa watu na kupelekea kukosa
uwajibikaji na uwazi kwa baadhi ya mamlaka husika,hivyo waandishi wa habari
wanakosa uwajibikaji na uwezo wa kufuatilia na kuhoji utendaji wa Serekali na
taasisi nyengine.
“Patakapo
kuwa na sheria zilizo rafiki za habari kutapelekea kupata mabadiliko ya nchi
hasa katika tasnia ya habari pamoja na maendeleo katika nchi, kwani kutakuwa na
misingi bora ya sheria ambazo zinatoa uhuru kwa kila mtu, na zitapelekea kukuza
uwajibikaji na uwazi wa Serekali,hivyo waandishi wa habari watapata uwezo wa
kufuatilia na kuhoji utendaji wa Serekali na taasisi nyengine kwa ufanisi
zaidi”ameeleza Mwanasheria.
Kwa ujumla
mabadiliko ya sheria za habari zina
uwezo mkubwa wa kubadilisha tasnia ya habari kuwa chombo imara cha maendeleo
,haki na demokrasia pamoja na kuweka mazingira mazuri ya sheria ,habari
zinaweza kufikishwa hadi maeneo ya vijijini na kwa makundi yasiyokuwa na sauti,kama
wanawake ,watu wenye ulemavu na vijana ambapo itapelekea kupata maendeleo
katika nchi na taifa kwa ujumla,hivyo basi ni vyema kwa Serekali ,wadau wa
sharia,pamoja na mamlaka zote zinazohusika kuifanyia kazi sharia ya habari mpya
ambayo itakwenda na misingi ya tasnia ya habari nchini.
0 Comments