Na
Siti Ali, Zanzibar:
Sekta ya habari kwa kiwango kikubwa kina mchango
mkubwa katika jamii kwenye kuleta mabadiliko
na maendeleo ,haki na wajibu lakini pia
inashughulikia tatizo kubwa la hadhi ya wanahabari ambayo ni kuifanya kazi ya
habari iwe taaluma ambayo kipato chake kinaelezeka kwa mujibu wa sheria.
Sheria pia ina
mchango mkubwa katika sekta ya habari kwani imetoa fursa na uhuru kwa kila mtu
kujieleza,kutoa taarifa ,kupokea taarifa,kulingana na katiba ya jamuhuri ya
muungano wa tanzania (ibara ya 30 na
ibara ndogo ya 5) ambayo inasema furahiya haki zako lakini usiharibu
amani,maadili usalama wa watu pamoja na maslahi ya umma,hii inatokana na uhuru
wa kujieleza kwa kufuata sheria zinazowaongoza wanahabari.
Taasisi za kimataifa ambazo zinafanya tathmini ya hali
ya kidemokrasia ,uhuru wa habari na kujieleza ,zinatumia taarifa za sasa baada
ya mabadiliko na kufanya tathmini.
Maana wamekuwa wakitumia taarifa za muda mrefu na
kuifanya nchi kuonekana imepiga hatua katika sheria ya habari,uhuru wa wanahabari na kutanua wigo wa demokrasia.
Licha ya kuwepo mafanikio mbali mbali ya sheria katika
sekta ya habari lakini pia zipo changamoto za sheria ambazo zinaikabili sekta
ya habari ambazo zinarudisha nyuma uhuru wa habari kama ifuatavyo :
Sheria ya uhuru wa habari zanzibar katika katiba ya
mwaka 1984 kama inavyosomeka ibara ya 18
(1)Bila ya kuathiri sheria nyengine za nchi,kila mtu anayo haki ya uhuru wa
maoni (kujieleza),kutafuta,kupokea na kusambaza habari na mawazo yake kupitia
chombo chochote cha habari bila ya kujali mipaka ya nchi na pia anayo haki na
uhuru wa kutoingiliwa mawasiliano yake. Ambapo sheria hii inampa mwandishi wa
habari fursa ya kutoa na kusambaza ujumbe kwa jamii ikiwa ndio lengo halisi la
mwandishi wa habari.
Sheria nyengine ni sheria ya Tume ya Utangazaji na.7
ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho na sheria na.1 ya Mwaka 2010.ambapo
sheria hii inampa fursa ya mwandishi wa habari kufanya kazi lakini pia sheria
hii sio rafiki kwani haimlindi mwandishi wa habari katika kazi yake.
Sheria ya Wakala wa Usajili wa Wakala wa Habari,
Magazeti na Vitabu na.5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria na.8
ya mwaka 1997.ambapo pia sheria hii licha ya kufanyiwa marekebisho lakini pia
ina mapungufu ambayo yanamuathiri
mwandishi wa habari katika kufanya majukumu yake ya kila siku,ni vyema
mamlaka husika kulifanyia kazi suala hili kwa haraka ili kumaliza kilio cha
waandishi wa habari.
Mwandishi wa habari kutoka gazeti la Chanzo Najjat Omar amesema kuwa sheria ya habari ina mchango
mkubwa katika kuleta miongozo na kufuata mambo mbali mbali ingawa bado zipo
sheria ambazo zimekuwa na changamoto nyingi ambazo zinamkwaza mwandishi wa
habari katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
“Sheria ina mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko
katika nchi kwani nchi yoyote haiwezi kwenda bila ya sheria ambayo inatoa
miongozo mbali mbali hivyo natoa wito kwa Serikali isikilize kilio cha
waandishi wa habari kuupitisha muswaada wa sheria ili kupata unafuu mkubwa
katika kuisadia Serikali kuleta demokrasia na amani ya nchi”ameelezea Najjat Mwandishi wa habari
Mwandishi wa habari wa kujitegemea Ali Vuai Kombo,anasema kuwa sheria ya habari ina mchango mkubwa katika
kusimamia majukumu ya wanahabari na utekelezaji wa muandishi wa habari kwenye
kazi zake pamoja na kulinda haki za jamii kupitia vyombo vya habari hivyo ni
wazi kuwa mchango wa sheria ni mkubwa kulingana na maendeleo yaliopo katika
nchi.
“Mchango wa sheria ni mkubwa kulingana na mabadiliko
ya nchi kwani mwandishi wa habari anatakiwa kufuata maadili yake ambayo ni kama
sheria itakayo muwezesha kufanya majukumu yake ya kila siku ambayo yanamsaidia
kuleta maendeleo katika nchi na taifa kwa ujumla”amesema Ali Vuai.
Mwanasheria Juma Khamis Juma amesema kuwa sheria ina
mchango mkubwa katika sekta ya habari kwani ni muhimu katika maendeleo ya
nchi,pia na kusema kuwa nchi yenye sheria sio tu ya habari bali hata sheria
nyengine ndiyo yenye nafasi ya kupiga hatua mbele katika kuleta mabadiliko na
maendeleo.
“Sheria ina mchango mkubwa katika sekta ya habari
kwani ni muhimu katika maendeleo ya nchi,kwani nchi yenye sheria sio tu ya
habari bali hata sheria nyengine ndiyo yenye nafasi ya kupiga hatua mbele
katika kuleta mabadiliko na maendeleo”anaelezea Mwanasheria Juma.
Licha ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali zinzogusa
sheria ya habari hapa Zanzibar lakini bado kuna hatua tofauti zinazochukuliwa
na Serekali katika kutatua kilo cha waandishi wa habari cha kulipitisha sheria
mpya ya habari ambayo inakwenda kuikomboa sekta ya habari na uhuru wa habari.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mh Tabia
Maulid Mwita wakati akizungumza na Maafisa habari tarehe 4 aprili katika ukumbi
wa New Amani Comples amesema katika kipindi kijacho Serikali inatarajia kuisoma pamoja na kuipitisha sheria ya habari
ambayo itasaidia kuleta mabadiliko katika nchi na taifa kwa ujumla.
“Kipindi kijacho Serikali inatarajia kuisoma pamoja na kuipitisha sheria mpya ya
habari ambayo itasaidia kuleta mabadiliko wanahabari pamoja na taifa kwa ujumla”ameelezea
Waziri Tabia.
Katibu wa Clabu ya waandishi wa habari zanzibar (ZPC)Mwinyimvua
Abdi Mzukwi amesema kuwa sheria ya habari ina mchango mkubwa kwani inasaidia
kuongeza uwajibikaji kwa waandishi pamoja na kulinda maslahi mwandishi.
“Sheria ikiwa rafiki kwa waandishi kutapelekea
kuongeza ari na mori kwa waandishi kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuwajibika
ipasavyo kwenye majukumu yao kwani kufanya hiivyo kutapelekea kupata mabadiliko
katika sekta ya habari na maendeleo katika nchi”Mwinyimvua anaeleza.
Afisa Program kutoka Chama cha Waandishi wa Habari
Wanawake Tanzania (TAMWA -ZNZ) Zaina Abdallah Mzee anasema kuwa sheria zilizopo
zikifanyiwa marekebisho na zitaweza kuondoa woga kwa waandishi wa kukusanya na
kuripoti habari na kuiwezesha jamii kupata taarifa kwa wakati .
“Kwa kipindi kirefu tumeendelea na kufanya uchechemuzi
lakini marekebisho ya sheria kuu mbili yaani Sheria ya Wakala wa Habari
Magazeti na Vitabu ya Mwaka (1988)na sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar ya mwaka (1997)ambazo waathirika wakubwa ni
waandishi,vyombo vya habari na jamii iliyotuzunguka “ameeleza Afisa huyo.
Kwa ujumla sheria ina mchango mkubwa katika kuendeleza
sekta ya habari na kuleta mabadiliko katika nchi, kwani Mwandishi wa habari
akifuata maadili ya uwandishi wa habari ataweza kufanya kazi zake bila ya
kupata usumbufu katika kazi zake.
Hivyo ni vyema kwa waandishi wa habari kufuata sheria
na maadili katika kazi zao ambazo zitawasaidia
katika kutatua migogoro binafsi na kuleta maslahi ya taifa.
0 Comments