Na
Siti Ali, Zanzibar
MABADILIKO
ya
Sheria ya Habari yanaweza kuongeza uhuru wa kujieleza ,haki na wajibu lakini
pia huenda kushughulikia tatizo la hadhi ya wanahabari, ambayo itawafanya
waandishi wa habari kupewa kipao mbele na kuheshimiwa kama zilivyo kazi
nyengine, pamoja na kuifanya kazi ya habari iwe taaluma muhimu,taaluma ambayo
ina kipato kinachoeleweka kwa mujibu wa sheria .
Hali hii imebainika kutokana na waandishi wa habari
kukosa sheria rafiki kwao na kupelekea kukosa uhuru katika kazi zao na
kupelekea kukosa ufanisi wa kufanya kazi
zao.
Miradi mbali mbali inayohusu maendeleo inapatikana
kutokana na vyombo vya habari, kwani hupata fursa ya kutangaza changamoto
zilizopo na inapelekea maendeleo katika nchi.
Mwandishi wa Habari kutoka Gazeti la Chanzo Najjat
Omar anasema sheria hizi zikifanyiwa mabadiliko kutakuwa na matarajio mazuri
kwa sababu wadau wa maendeleo wataleta miradi mikubwa sana ya nchi na serikali itapata fedha nyingi kwa kuwa kutakuwa na uhuru wa kulinda habari na wanahabari kwa ujumla.
“Matarajio yangu kama mwandishi wa habari kuona
serikali inanipa nafasi ya kubadilisha sheria kandamizi na ngumu ambazo
zinarejesha nyuma sekta ya habari”anaeleza Najjat.
Aidha Najjat amesema kuwa anatajia kuona kizazi cha
sasa na kijacho kinapigania misingi ya haki ,maendeleo na kufuata sheria mpya
zitakazowekwa na kufuata demokrasia pamoja na kutoona sheria kandamizi
zilizopita nyuma.
“ Matarajio yangu ni kuona kizazi cha sasa na kijacho
cha uandishi kinapigania misingi ya haki
,maendeleo na kufuata sheria mpya zinazowekwa za demokrasia pamoja na kutoona sheria kandamizi zilizopita
nyuma na kuwa mashujaa katika kulinda mikataba ya haki za binaadamu,mikataba ya
sheria na yote iliyosainiwa na Serekali hususani katika Serekali ya awamu hii
ya nane chini ya uongozi wa Mh Rais Hussein Ali Mwinyi pamoja na waziri wa
habari vijana utamaduni na michezo Mh Tabia Maulid Mwita”Najjat amesema.
Mwandishi wa habari kutoka Daillynews Maryam Said amesema iwapo kutakuwa na sheria
rafiki za habari ,mabadiliko kadhaa chanya katika tasnia ya habari bali na
jamii kwa ujumla yanaweza kutokea
ikiwemo uwazi na uwajibikaji kuboresha utendaji wa taasisi za Serekali
kuimarika kwa ubora wa habari, ambapo waandishi watafanya kazi bila ya hofu
,hivyo habari zitakuwa za kina ,zenye uchunguzi ,na zenye ukweli zaidi itapelekea mafanikio katika nchi.
“Kuwepo kwa sharia rafiki kutaleta mabadiliko chanya
katika tasnia ya habari yanaweza kutokea ikiwemo uwazi na uwajibikaji pamoja na
kuboresha utendaji wa taasisi za Serekali ambapo waandishi watafanya kazi bila
ya hofu ,hivyo habari zitakuwa za kina ,zenye uchunguzi ,na zenye ukweli Zaidi ambapo itapelekea mafanikio katika
nchi.”ameeleza Maryam.
Waziri wa
Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mh Tabia Maulid Mwita wakati akizungumza na
Maafisa Habari tarehe 4 Aprili katika Ukumbi wa New Amani Complex amesema
katika kipindi kijacho serikali inatarajia
kuisoma pamoja na kuupitisha Mswaada wa Sheria ya Habari ambayo
itasaidia kuleta mabadiliko katika nchi na taifa kwa ujumla.
“Serikali ipo katika mkakati wa kuisoma sheria mpya ya
habari ya Zanzibar na tunatarajia kuipitisha na kuupeleka mswada katika Baraza
la Wawakilishi ili tuweze kuipata sheria mpya yenye kuaminika itakayotumiwa na
maofisa wa Habari”anaeleza Waziri Tabia.
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC)
Mwinyimvua Abdi Nzukwi anasema kuwa wanatarajia sheria rafiki za habari zitakazokuwapo
zitatoa uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko katika tasnia ya habari,tasnia ya
habari kuwa kichocheo cha maendeleo,haki na demokrasia katika nchi kwani
wananchi watajihisi salama kutoa maoni yao kupitia majukwaa ya habari na
kupelekea ustawi wa jamii pindi watakapotoa maoni yao.
“Tunatarajia kuwapo kwa sheria rafiki za habari ambazo
zitapelekea kupata mabadiliko katika tasnia ya habari, tasnia ya habari kuwa
kichocheo cha maendeleo ,haki na demokrasia katika nchi kwani wananchi
watajihisi salama kutoa maoni yao kupitia majukwaa ya habari na kupelekea
ustawi wa jamii”anaeleza Mwinyimvua Katibu wa ZPC.
Afisa programu wa masuala ya utetezi na uchechemuzi
kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA –ZNZ) Zaina
Abdallah Mzee anasema kuwa wanachukua jitihada za kuzisemea sheria zote zinazohusu
habari ambazo haziko huru, ili kusaidia kupata mabadiliko katika nchi, kwani kufanya
hivyo kutasaidia kupatikana maendeleo kwa haraka kwani wanahabari wakifanya
kazi zao vizuri Serikali itayakisi yaliyoko kwa wananchi na itapata fursa ya
kufanyia kazi kwa maslahi ya nchi.
“Tunachukua jitihada ya kutetea na kufanya uchechemuzi
wa sheria zilizopo za habari ambazo haziko rafiki kwa waandishi wa habari na
vyombo vya habari ili zirekebishwe na tunatarajia sheria mpya zitakazo kuwapo zitakwenda na misingi imara ya
haki,wajibu,na uhuru na ulinzi kwa waandishi na vyombo vya habari ili mchango
wao katika maendeleo ya nchi uonekane na utambulike ,”anaeleza Zaina.
Mwanasheria wa kujitegemea ndugu Muhammed Faki Khatib
anasema kuwa kuwapo kwa sheria rafiki za habari kwa waandishi wa habari kutapelekea
kupata mabadiliko makubwa nchi hasa katika tasnia ya habari pamoja na maendeleo
katika nchi, na taifa kwa ujumla.
Hii inatokana na kuwepo kwa misingi bora ya sheria
ambazo zinatoa uhuru kwa kila mtu ambazo zitapelekea kukuza uwajibikaji na
uwazi wa Serikali,hivyo waandishi wa habari watapata uwezo wa kufuatilia na
kuhoji utendaji wa Serikali na taasisi nyengine kwa ufanisi zaidi.
“Patakapo
kuwa na sheria zilizo rafiki za habari kutapelekea kupata
mabadiliko makubwa ya nchi hasa
katika tasnia ya habari pamoja na maendeleo katika nchi, na taifa kwa ujumla.
Itakapokuwapo misingi bora ya sheria ambazo zinatoa uhuru
kwa kila mtu, ambazo zitapelekea kukuza uwajibikaji na uwazi wa Serikali,hivyo
waandishi wa habari watapata uwezo wa kufuatilia na kuhoji utendaji wa Serikali
na taasisi nyengine kwa ufanisi zaidi”anaeleza Mwanasheria.
Kwa ujumla mabadiliko ya sheria za habari zina uwezo mkubwa wa
kubadilisha tasnia ya habari kuwa chombo imara cha maendeleo ,haki na
demokrasia pamoja na kuweka mazingira mazuri ya sheria ,habari zinaweza
kufikishwa hadi maeneo ya vijijini na kwa makundi yasiyokuwa na sauti,kama
wanawake ,watu wenye ulemavu na vijana ambapo itapelekea kupata maendeleo
katika nchi na taifa kwa ujumla.
0 Comments