![]() |
Waziri wa Nchi OR Fedha na Mipango Mhe. Sada Mkuya akiapa mbele ya Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kuwa mjumbe wa tume ya Mipango |
NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR:
Wanawake wengi hushindwa kufanya maamuzi ya kisiasa kwa sababu ya hofu ya kutopata msaada au kupata dhihaka kutokana na ushiriki wao katika siasa.wahenga wanasema mwanamke amekuwa kama ndege aliyekatwa mbawa zake hii inamanisha kuwa mwanamke anapokatishwa tamaa katika juhudi zake za kuwa kiongozi, anajikuta akipoteza ujasiri wa kuendelea na safari hiyo.
Licha ya kuwa baadhi ya mataifa mengine duniani yanatambua umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika nafasi ya uongozi na kuchukua hatua mbalimbali ya kisheria, kijamii, kiuchumi ili kuhakikisha wanawake wanapata nafasi nzuri katika siasa.
Mfano wa mataifa hayo ikiwemo Norway imekuwa mfano bora ya kutoa nafasi kwa wanawake ya ushiriki katika siasa, kupitia sheria ya kota ya mwaka 2023 inahakikisha kuwa asilimia 40% ya viti vyenye bodi za makampuni ya umma vinashikiliwa na wanawake nahii inasaidia kuongeza wakilishi wa wanawake katika maeneo ya biashara na usimamizi wa kampuni.
Hata hivyo , katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, imeweka wazi kuwa kila mzanizbar anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika mambo yanayohusu taifa lake na katika marekebisho ya 2010 imeeleza kutakuwa na wajumbe wa Baraza La Wawakilishi (BLW) asilimia 40 wa wajumbe kwa kila jinsia.
Hivi sasa ziaonekana zinafanyika jitihada mbalimbali za kurekebisha dosari hizi ili kuhakikisha mwanamke, anakuwa ni sehemu ya uongozi, ikiwemo kwenye mambo ya kisiasa kwa vile huko ndiko anapofanyika maamuzi muhimu ya kisiasa na kiuchumi.
Amanda Ameir ambae sio jina lake sahihi, mkaazi wa mwanyanya, aliyetamani kugombea nafasi ya jimbo lakini hofu imemtawala moyoni mwake na kushindwa kugombea nafasi hiyo.” Natamani sana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi hasa kwenye jimbo lakini hofu yangu ipo kwenye vitisho vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo rushwa ya ngono.”Amesema Amanda
“Katika harakati zangu za kisiasa ,nishawahi kukumbana na changamogo ya rushwa ya ngono wakati nagombea nafasi ya wasomi mwaka 2020 na kutobahatika kupata nafasi hiyo na miongoni mwa sababu ya kutopata nafasi hiyo ikiwemo kutokuwa na uwezo wa kufanya kampeni pamoja na kushawishiwa rushwa ya ngono, hali hii ilinifanya nichukie kujishirikisha katika nafasi mbalimbali za kisiasa.” Ameongezea Amanda
Waziri wa Nchi Ofsi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Sada Mkuya amesema ametumia njia mbalimbali katika kugombea nafasi ya jimboni ,wakati baadhi ya wanawake wanaogopa kuingia jimboni .” kiukweli safari ya kuingia katika jimbo inahitaji ujasiri, uvumilivu na ukakamavu ambao unamsaidia mtu kufika pale anapotaka, kwahiyo mimi niliweza kujiamini na kuondoa hofu ndani ya moyo wangu na nikajiandaa kimapambano na zaidi nilitaka kuwaonesha wanaume kuwa nasi tunaweza kushiriki nafasi mbalimbali .”Amesema Dkt Sada Mkuya
“Mwaka 2015 niligombea nafasi ya ubunge katika jimbo la welezo nakwabahati nzuri nilifanikiwa kushinda, na sababu kuu ilionifanya nishinde ni kuwa na mashirikiano na watu vizuri ikiwemo watoto, vijana hadi wazee ,kuweza kujiamini,pamoja na kufanya jitihada ya ufanyaji wa kampeni, hivyo baadhi ya wanawake wanaogopa kuingia jimboni kwasababu ya hofu hii inatoka na jamii kutoweza kubadilika kwa kuamini mwanaume ndio anaestahili kushika nafasi za uongozi hivyo jamii ibadilike.”Amesema Sada Mkuya
Tume ya Uchaguzi Zanzibar inamchango gani kuhakikisha wanawake wanashiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi, na kukutana na Mkurugenzi wa Tume hiyoThabit Idarous ,” Wanawake wamepewa fursa mbalimbali za kugombea uongozi katika tume ya uchaguzi Zanzibar ,tatizo lipo wanawake wenyewe hawajitokezi kuchukua fomu ya kugombea ukiangalia katika mwaka 2015 hadi 2020 wamejitokeza wanawake 80 kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo uwakilishi, ikilinganishwa na wanaume zaidi ya 400 waliojitikeza kugombea nafasi hiyo.” Amesema Thabit
“ Takwimu za uchaguzi wa mwaka 2020 kwa upande wa Zanzibar wabunge walioteuliwa na vyama kugombea nafasi hiyo wanaume 257 ambapo wanawake walikuwa 81 hii inaonesha wazi kuwa bado muamko wa wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi bado ni mdogo kutokana na woga uliowakabili.” Ameongezea Thabit
Amependekeza elimu itolewe kwa wingi kwa wanawake ili kuweza kupata muamko na kuondoa woga unaowakabili na kuwashauri vyama vya siasa kuwapa kipaumbeke wanawake katika kushika nafasi mbalimbali za uongozi .
Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tamwa – Zanzibar kinatoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake na kutatua changamoto zinazowakabili, hivyo mwaandishi alikutana na mkurugenzi wa chama hicho ili kujua vipi wanaweza kuwasaidia wanawake wanaotamani kuingia katika nafasi ya jimbo lakini wanaogopa.”Tumetoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake zaidi ya 100 na tukagundua asilimian 70 ya wanawake wanachangamoto ya hofu ambayo inawafanya kushindwa kugombea nafasi ya jimbo.” Amesema Dkt Mzuri
“Ukiangalia wawakilishi wa majimbo 50 Zanzibar wanawake 8 sawa na silimia 16, wabunge wa jamuhuri ya muungano kutoka Zanzibar kwenye majimbo 50 wanawake wanne,sawa na asilimia 8 ,mawaziri 6 sawa na asilimia 33 ,makatibu wakuu 7 sawa na asilimia 39 hii inaonesha idadi ndogo ya wanawake kushiriki nafasi mbalimbali za uongozi kutokana na hofu ya kuweza kutojiamini.” Amesema Dkt Mzuri
Katibu Mkuu wa Chama Cha Kidemocrasia Cha Watu wa Umoja UPDP Hamad Ibrahim amesema kwa mujibu wa katiba ya chama chao imetoa nafasi kwa wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, Mfano halimashauri kuu ya chama chao inawashiriki 25 wanawake 9 na wanaume 16 nasio kama tumependa kuweka idadi hii kwa wanawake tatizo wanawake wenyewe hakuweza kujitokeza kutokana na woga uliokithiri moyoni mwao.” Nikweli wanawake hutamani kugombea nafasi mbalimbali lakini hofu ndio kikwanzo kinachowafanya kushika nafasi ya mbalimbali ikiwemo nafasi ya jimbo.”Amesema Hamad
“Wanawake wanavigezo vingi sana katika nchi yetu, tatizo lipo wanapoangalia madhaifu ya nyuma kwa hiyo wanatakiwa kuachana nayo na waangalie mafanikio ya wanawake wengine na endapo watafanyiwa vitendo vya udhalilishaji wasiache kusema ili wajulikane wanaochochea vitendo hivyo na adhabu itolewe, kwahiyo wanawake wanatakiwa kushiriki kwa wingi, kwani wao ni waaminifu sana katika masuala ya uongozi kuliko wanaume endapo wakijitokeza kwa wingi uchumi wa nchi utazidi kuimarika.” Ameongezea Hamad
Ripoti ya mwaka 2018 inayohusu uwiano wa kijinsia ulimwenguni imeweka picha halisi ya haki za wanawake katika siasa, uchumi na elimu ili kuutanabahisha ulimwengu kasoro ziliopo na kuelezea umuhimu wa kufanyika marekebisho.
0 Comments