Chama cha ACT-Wazalendo kimerichia kushiriki katika
serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na kuwaruhusu wateule wote wa chama hicho
waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 na 29 mwezi Oktobar
kushiriki katika vyombo vya maamuzi walivyochaguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari huko katika ofisi
za chama hicho Magomeni, jijini Dar-es-salaam katibu mkuu wa chama hicho ndugu,
Ado Shaibu alisema wamefikia maamuzi mara baada ya kutafakari kwa kina juu ya
mwenendo wa siasa za Zanzibar na Taifa kwa ujumla.
”tunafanya uamuzi huu kwa ajili ya maslahi ya
wazanzibar,maslahi ya taifa pamoja na maslahi ya chama chetu” alisema katibu
mkuu huyo
Alisema chama cha ACT-Wazalendo kilifanya ziara katika
maeneo mbalimbali na Zaidi katika maeneo ambayo yaliathirika kwa kiasi kikubwa
katika uchaguzi mkuu ili kusudi kusikiliza maoni yao juu ya suala la kushiriki
au kutokushiriki katika Serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar ambapo asilimia
kubwa ya wanachama waliridhia chama hicho kushiriki katika Serikali hiyo pamoja
na kuwaruhusu wateule wote wa chama hicho ambao ni wabunge,wajumbe wa baraza la
wawakilishi pamoja na madiwani kuzitumikia nyadhifa walizochahuliwa.
”tumepata muda mrefu wa kufanya tafakuri ya kina
lakini pia kamati kuu imekwenda kuwasikiliza wanachama hasa katika maeneo
ambayo wamepata madhila makubwa katika uchaguzi huu juu ya jambo hili
ambapo wameridhia tuwaruhusu wawakilishi
wetu washiriki katika vyombo vya uwakilishi na pia tushiriki katika Serikali ya
umoja wa kitaifa Zanzibar” aliongezea ndugu Ado Shaibu
Aidha katika hatua hio
chama cha ACT-Wazalendo wameiomba Serikali ya kitaifa itakayoundwa kutekeleza
mambo mbalimbali ikiwemo kufanyika kwa uchunguzi wa matukio yote yaliyotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi
ya uvunjaji wa haki za binaadamu na kuwafariji waathirika wote pamoja na
kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika kupanga na kutekeleza matukio hayo, Kunafanyika Mabadiliko
ya mfumo wa Uchaguzi Zanzibar ili kurejesha imani ya wananchi juu ya uwepo wa
uchaguzi huru na wa haki.
Pamoja na Kunafanyika
Marekebisho ya uendeshaji wa vyombo vya Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar ili vifanye kazi kwa Weledi na bila ubaguzi wa kisiasa.
“Dhima ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kwa maslahi ya
Wananchi inapaswa pamoja na mambo mengine ihakikishe kuwa, inachunguza wa
matukio yote yaliyotokea kabla, wakati na baada ya Uchaguzi ya uvunjaji wa haki
za binaadamu, unafanyika na kuwafariji waathirika wote pamoja na kuwachukulia
hatua za kisheria waliohusika kupanga na kutekeleza matukio hayo” Alisisitiza
katibu mkuu huyo
Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi mkuu wa 2020
chama cha ACT-Wazalendo kilipata asilimia 19.87% ambapo
kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar kinaruhusiwa kupendekeza jina la makamu wa kwanza
wa Raisi wa Zanzibar.
1 Comments
Ni hatua nzuri kwa Zanzibar na taifa kwa ujumla
ReplyDelete