Ticker

6/recent/ticker-posts

Wadau Wataka Juhudi Za Ushiriki Wa Wasichana Na Watu Wenye Ulemavu Kwenye Michezo Ziongezwe




NaNajjat Omar, Zanzibar:


Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto – UNICEF kupitia ripoti zake kadhaa inaonesha ushiriki wa wasichana na watu wenye ulemavu kwenye michezo ni mdogo hii inaweza kufikia asilimia 10 hadi 20 ila kwenye mazingira wezeshi yenye miundombinu inaweza kufika hadi asilimia 50 kwa 60.


Ripoti hizo zinaonesha ongezeko hilo kuwa juu zaidi kwa nchi ambazo zimeweka malengo kwenye michezo kwa wasichana na watu wenye ulemavu kama Afrika Kusini,Kenya na hata Nigeria kwa kufikia hadi asilimia 30 mpaka 50 kwenye ushiriki.


Ikiwa michezo na ujumuishwaji wa masuala ya Maendeleo ni suala ambalo lipo katika utekelezaji wa dira wa Maendeleo ya Zanzibar ila bado kuna changamoto zinawakabili wasichana na watu wenye ulemavu kwenye kushiriki michezo.


Riziki Islah ni Kocha na muwezeshaji wa masuala ya kimichezo kwa kuzingatia ujumuishi amesema suala na ushiriki wa wasichana linaonekana ila kila hatua ambayo msichana anazidi kukua ndoto zake za kimichezo zinapotea. 

”Tumekutana hapa kuzungumza na kujadili pia kupeana elimu juu ya kuendelea kushirikiana na jamii kwa kutoa Elimu lakini pia kuwasaidia jamii kwenye Elimu hii hata kuwashirikisha kwenye masuala ya kimichezo ili juhudi za wasichana na wanawake ziongezeke na ndoto zao zitimie”Amesema Riziki wakati akizungumza na mwandishi wa Makala hii.


Tahir Aboubakar ni Kocha wa mpira wa miguu wa Timu ya watu wenye ulemavu akiwa mmoja wa watu wenye ulemavu wa mkono haijampa sababu ya yeye kuacha kuendeleza ndoto zake wa kuwa golikipa kati timu kadhaa hapo awali na hadi sasa kuwa mwalimu wa timu za wasichana chini ya umri wa miaka 12 hadi 15.

”Jamii inanichukulia kuwa kutokana na hali yangu kwamba siwezi kufundisha kitu ambacho ni tofauti “ Amesema Tahir huku akiendelea kutoa wito kwa Serikali na jamii “Kwanza tuache dhana ya kuwaficha na sisi timu yetu inapokea na kuwasomesha watu wenye ulemavu masuala ya michezo waje pale Maisara au hapa Mnazi Mmoja ili kujiunga nasi na sio kuwaficha kabisa kushiriki michezo hii ni haki ya kila mtu “ Amemaliza Tahir.


Utafiti uliofanywa na Shirika na Maendeleo la Ujerumani hapa Zanzibar unaona ni robo tatu na wasichana ndio hushiriki katika michezo huku vikwazo vikitajwa ni masula ya iman na Elimu duni.



Neema Machano ni  Katibu wa soka la Wanawake hapa visiwani Zanzibar licha ya kuwa mchezaji mpira anakiri kuwepo kwa dhana ya uhuni kwenye michezo kwa wasichana jambo ambalo anapingana nalo kwa kusema malezi ndio humbadilisha au kumuacha msichana na tabia zake na sio mpira

”Kwa sasa kuna mabadiliko makubwa kwenye taratibu na kanuni za kucheza mpira wa miguu kwa wasichana kwa sasa ni lazima ujisitiri ndio ucheze na sio kuvaa wazi,dhana ya uhuni ni malezi na mtu mwenyewe na sio kushiriki michezo”

Ameendelea kusema “Fursa za kimichezo kwa wasichana kwa sasa ni nyingi licha ya kwamba ni lazima kuwepo kwa miundombinu na mbinu za kuzifikia hizo fursa serikali iliangalie hili kwa ukubwa wake” Amesema Neema Machano.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar -ZFF linajukumu la moja kwa moja kuwasaidia na kuwasimamia wasichana na watu wenye ulemavu kushiriki michezo ,Ali Mohammed Ali ni mjumbe wa kamati ya soka la Wanawake kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar -ZFF amesema juhudi wanazozichukua kwa sasa ni kuanza kutoa Elimu kwenye maskuli na hata vilabu juu ya kuondoa dhana potofu kwenye masuala ya michezo.

”Kiuhalisia kwa mazingira yetu ya Zanzibar tunaelewa mdogo kidogo kuhusu masuala ya michezo kwa wazee,tukimaliza maskuli kutoa Elimu tutafikisha Elimu hio kwa jamii hususani wazee “ Amesema Ali Mohameed.


Jukumu wa kuwasaidia wasichana na watu wenye ulemavu kushiriki masula ya michezo ni la jamii, wadau na serikali,Khadija Majaaliwa Juma ni Afisa Michezo Wilaya ya Mjini amesema serikali inasaidia watu wenye mahitaji maalum kucheza na kushiriki masuala ya kimichezo ,huku utambuzi wa vyama vyao ukitambulika ,pia kupatiwa nafasi za uongozi kwenye sehemu kubwa za kimichezo.

”Ni vyema wadau watambue kuwa sio wanajamii wote wenye Elimu ya masuala ya kimichezo ,sasa serikali na wadau watoe  Elimu kwa jamii kwamba wasichana na watu  wenye mahitaji maalum wasitengwe kwenye ushirikishwaji wa michezo”

Amewataka wadau pia kujitokeza kuwawezesha na kutoa msaada wa mafunzo na Elimu ya kujitambua kwenye kujisimamia na kuwa na uthubutu wa kuwasaidia wengine kwenye michezo.


Mradi wa masuala ya michezo na Maendeleo unaowawezesha waandishi wa habari 30 kutoka Pemba na Unguja unatekelezwa na Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Zanzibar – TAMWA -Z  kwa ushirikiano wa  Serikali ya Ujerumani kwa mashirikiano ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la kutoa Elimu na kuongeza ujumuishaji wa Wanawake,wasichana na watu wenye ulemavu kwenye sekta ya michezo.

Post a Comment

0 Comments