Wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya ya Kusini wameshauri fedha za mfuko wa jimbo zinazotengwa kwa wabunge na wawakilishi kwa ajili ya kusaidia miradi ya maendeleo ya wananchi kuelekezwa katika miradi michache ambayo italeta tija na manufaa kwa jamiii
Wakizungumza mara baada ya kukagua miradi inayotekelezwa kupitia fedha hizo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Octoba 2023 hadi machi 2024 kwa jimbo la Paje na Makunduchi
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kusini Bi Asha Mzee Omar na Mwenyekiti Mohammed Hassan Haji wamesema kamati imegundua kuweko kwa baadhi ya miradi iliyopangwa kutekelezwa katika nusu ya kota inasuasua na mengine kushindwa kutekelezwa kabisa kwa sababu ya wingi wa miradi na fedha ni chache hali inayopelekea kutokamilika kwa wakati na wananchi kushindwa kunufaika na uwepo wa miradi hiyo.
Aidha wamesema ni vyema kwa wananchi wakaunga mkono juhudi zilizofikiwa na viongozi wao wa majimbo kwa kuthamini na kuitunza miradi hasa ya maji safi na salama kwa kuifukia miundo mbinu ili kuepukana na madhara mbali mbali ikiwemo magonjwa na kuharibiwa.
Nae Kaimu Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kusini Juma Mohammed Chande amesema imefika wakati kwa viongozi wa majimbo kushirikiana na kamati za maendeleo kuhakikisha wanaibua miradi michache ambayo yana tija na yenye kwenda sambamba na kiwango cha fedha zinazoingizwa kwenye mfuko wa Jimbo kwa kila mwaka.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa nyumba ya daktari Mtende, ukarabati wa banda la skuli ya Kiongoni Makunduchi na mradi wa maji safi na salama Jambiani
0 Comments