Ticker

6/recent/ticker-posts

Madiwani Wanawake Wanavyoibua Hoja Za Kuanzishwa Miradi Ya Kimaendeleo

 

Mradi wa ujenzi wa Maegesho ya Gari Michamvi

Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:


Mapambano ya kuhakikisha wanawake anafikia lengo la kuwa kiongozi kwenye ngazi mbalimbali bado yanaendelea.

Hii inatokana na matumaini kwa jumuiya zisizo za kiserikali zinazopigania usawa wa kijinsia kwenye uongozi na demokrasi visiwani Zanzibar kuona mwanga wa mafanikio juu ya nafasi ya mwanamke kwenye eneo hilo.

Moja ya maeneo ambayo yameanza kuleta mwanga ni baraza la madiwani Wilaya ya kusini.

Baraza hilo lina wajumbe nane, sita kati yao wakiwa ni wanawake na wawili wakiwa ni wanaume.

Lakini uwepo wa idadi kubwa kwenye baraza hilo inaleta faida gani kwa baraza hilo na wananchi wa Wilaya hiyo?

 

Mwenyekiti wa Baraza hilo Mustafa Mohammed Haji ambaye pia ni Diwani wa wadi ya Muyuni alisema madiwani wanawake kumekuw na mchango mkubwa katika kuibua miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo Kiwanja cha Kufurahishia watoto kinachoendelea kujengwa Paje, Stebi ya Magari Michamvi pamoja na Masoko yaliyojengwa maeneo mbalimbali.

“Wanawake hawa wamekuwa mstari wa mbele katika katika kuchangia mikakati ya kuona tunapata fedha za kukidhi mahitaji ya miradi ambayo tumejipangia kwenye Bajeti ya mwaka husika” Alisema

Vilevile Mwenyekiti huyo alisema madiwani wanawake wa baraza hilo wamekuwa wafuatiliaji wakubwa wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia muda na ubora wa miradi hiyo.

“kamati nyinyi za baraza kuna madiwani wanawake kwa hivyo ule uharaka wao wa kuwaelekeza watendaji wafikekwenye eneo la Mradi inawafanya hata watendaji wawe na kasi ya uwajibikaji kwenye miradi hiyi” Aliongeza

Zawadi Hamdu Vuai ni diwani wa wadi ya Kiongoni,  alisema wanawake ni binadamu kama walivyo  wanaume na wanamudu majukumu yote ya kiungozi katika maeneo wanayoongoza kwa kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuwanufaisha wananchi wanaowaongoza sambamba na kuleta ukombozi wa jamii zao.

“Jamii humtegemea kila mwenye uwezo, wanawake tunao uwezo mkubwa hasa kwenye usimamizi wa fedha za umma zinazolenga kujenga miradi” Alisema Diwani huyo

Aidha alisema suala la kuwa mwanamke anaweza kuongoza ama laa ni suala la kuangalia utendaji wa viongozi wanawake kwani matendo na matokeo chanya ya viongozi wanawake yanaonekana huku akiwataka wenye mtazamo kuwa wanamke hawezi kuongoza waondoe mtazamo huo.

Mda Mohammed Shaka ni Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Kusini yeye alisema kazi za kiutendaji ndio hizohizo wanazozifanya wanaume na wanazitekeleza kikamilifu ama zaidi ya hao wanaume huku akiiomba jamii kundoa hofu juu ya kuongozwa na mwanamke.

“Tunauwezo sawa au hata kuwashinda hao wanaume kwenye utendanji” Alisema

Upande wa diwani wa Viti Maalum Wilaya Ya Kusini Maulid Hassan Zidi alisema lengo lao ni kuibadilisha Halmashauri ya Wilaya ya kusini Kuwa Manispaa.

“Tunataka kuipeleka Halmashauri kuwa Manispaa na tunaamini kutokana na miradi tunayotekeleza kwa sasa tutafanikisha hilo” alisema

Kwa msingi huo inaonyesha kuwa wanawake wanaweza kuongoza endapo wataaminiwa na kupewa nafasi.

Hivyo ni jukumu la kila mmoja kwa nafasi yake anaanza kumuandaa mwanamke kiuongozi hata akiwa mtoto mdogo.

 

Post a Comment

0 Comments