Mbunge Wa wananchi wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa Chumbuni Bamita.
Baada
Ya Sala hiyo Pondeza Aliwasihi Waumini Kuungana kwa Pamoja kwa Kuendelea
Kufanya ibada jambo litakalosaidia kupata radhi za Mwenyezi Mungu.
“Malipo ya ibada zetu kwenye mwezi huu ni mara dufu ya malipo katika miezi mingine hivyo niwaombe tujitahidi kufanya ibada kwa wingi” Alisisitiza
Aidha Mbunge huyo aliushukuru Uongozi wa Wa Msikiti Wa Bamita Kwa Kuendelea Kuwapa Taaluma Ya Dini Ya kiislamu Jamii Ya Maeneo Hayo Kwa kuwafundisha Qur- an Watoto na watu wazima.
Kwa
upande wake Diwani Wa Wadi Ya Chumbuni Ambar
Ujudi Bamba aliwataka waumin Wa Maeneo Hayo Kuendeleza Amani Utulivu Na Upendo.
“Endapo
tutaimarisha amani na upendo miongoni mwetu itakuwa njia ya kuridhiwa na
Mwenyezi Mungu na Kupiga hatu za maendeleo” Alisema
0 Comments