Ticker

6/recent/ticker-posts

Dkt. Mzuri: Zipeni Kipaumbele Habari Za WanawakeNa Ahmed Abdulla:


WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kuandika habari zinazohusu Wanawake kuzingatia vigezo vya kiuandishi ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Upande wa Zanzibar TAMWA-ZNZ katika hafla maalum ya utoaji wa Tunzo za umahiri wa Uwaandishi wa habari za Takwimu iliyofanyika ukumbi wa Shaa Mjini Unguja.

Alisema endapo waandishi wa habari watajikita kwenye kuandika habari za matokeo chanya yanayofanywa na wanawake basi lengo la kufikia asilimia 50 kwa 50 kwenye nafasi za uongozi nchini litafikiwa.

“Tunaamini wanawake wanaweza kuwa active zaidi katika masuala ya uongozi endapo waandishi wa habari wataandika habari kuhusu wao” Alisema Dkt. Mzuri Issa

Mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Salum Kassim Ali yeye aligusia suala la vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto na kueleza kuwa, Takwimu zinaonesha kuongezeka kwa idadi ya vitendo vya udhalilishaji hivyo waandishi wa habari wanawajibu mkubwa kuendelea kuandika habari ili kuchangia mabadiliko chanya katika jamii juu ya vitendo hivyo.

“Takwimu kutoka ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali zinaoesha kuwa, mwaka 2020 jumla ya matukio 1360 yameripotiwa, 2021 matukio 1361, 2022 matukio 1366 huku mwaka 2023 matukio 1994 yameripotiwa ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia,” ameelezaa.

Aliongeza kuwa kwa mwezi wa Januari 2024 jumla ya matukio 1760 ya wanawake kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia yameripotiwa Zanzibar.

“Kiukweli idadi ni kubwa sana ya matendo haya ya udhalilishaji hivyo niwaombe ndugu zangu wanahabri kuongeza jitihada katika kuandika ili kuweza kupunguza haya matendo ambayo yanatia doa Zanzibar,” ameeleza.

Mapema Afisa kutoka Mamlaka ya kuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) Yusuf Juma Suleiman ameahid mashirikiano baina ya ZAECA na Waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao kila siku.

“Waandishi sis ZAECA tunaahidi mashirikiano na nyinyi kattika kutekeleza majukumu yenu hususani kuandika habari rushwa ya ngono ambayo nayo imekithiri,”ameeleza.

Jumla ya kazi 525 ziliwasiliswa kwa ajili ya kuwania tuzo hizo ambapo kwa upande wa waandishi wa Magazeti tuzo ilikwenda kwa Asya Mwalimu wa gazeti la Zanzibar Leo, waandishi wa Radio za kitaifa tuzo ilikwenda kwa Huwaida Nassor wa Radio Assalaam Fm, waandishi wa Radio za kijamii tuzo ilikwenda kwa Amina Massoud Jabir kutoka Radio Jamii Mkoani na Waandishi wa mitandao ya Kijamii tuzo ilikwenda kwa  Zuhura Juma Said huku msindi wa jumla akiwa ni Amina Massoud Jabir wa Radio Jamii Mkoani.

Post a Comment

0 Comments