Ticker

6/recent/ticker-posts

Muhanga Wa Kupingwa Na Mama Wa Kambo Bububu Yuko Salama

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Abeida Rashid Aballah akiwa na  mtoto Farhia Omar Mohamed (10) ambaye aliyekuwa anapigwa na mamaake wa kambo huko Bububu, Unguja na hatimae mtoto huyo kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzimbar, Kupitia Wizara hiyo


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Aballah amesema  mtoto Farhia Omar Mohamed (10) ambaye aliyekuwa anapigwa na mamaake wa kambo huko Bububu, Unguja hali yake inaendelea  vizuri.


Ameyasema hayo wakati alipomtembea mtoto huyo katika nyumba ya kulea watoto Mazizini, Unguja.


Bi Abeida amesema mtoto Farhia atapatiwa haki zake zote za msingi kama sheria  ya mtoto inavyoeleza .


Amefahamisha kwamba sheria ya mtoto sheria Na 2 ya mwaka 2011 imeainisha haki za mtoto ikiwemo haki ya kupata elimu, matibabu, kuishi, nk.


Ameeleza ni wajibu wa Wizara  ya Maelendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto  kusimamia utekelezaji wa sheria  hiyo kwa maslah ya taifa.


Aidha katibu Mkuu Abeida ametoa wito kwa  wazazi  na walezi kutumia busara zaidi wakati wa kumuadhibu mtoto endapo amefanya kosa, kwani ikumbukwe kwamba mtoto ni wa Serikali hivyo, Serikali haitovumilia kuona mtoto anafanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa aina yeyote ikiwemo kupigwa, kunyanyaswa, kutelekezwa, n.k.


Mtoto Farhia Omar alichukuliwa  na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na kuhifadhiwa katika malezi bora, siku ya Jumapili, tarehe 11/02/2024


Post a Comment

0 Comments