Ticker

6/recent/ticker-posts

Kamati Ya Wadau Wa Habari Bado Yalia Na Sheria Ya Habari Zanzibar



Kamati ya Wadau wa Habari Zanzibar (ZAMECO) imekutana kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya sekta ya habari,changamoto na hatua zilizofikiwa katika kuendeleza sekta hiyo muhimu katika ujenzi wa jamii inayozingatia usawa, maendeleo, haki za binadamu na inayojali misingi ya kidemokrasia.  



Katika taarifa iliyotolewa na kamati hiyo ilieleza kuwa Kikao hicho kilijadili kwa kina changamoto za sheria za habari Zanzibar na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wadau wa habari katika kutoa maoni hususan katika kufanya uchambuzi wa kina wa sheria hizo ambazo kwa kiasi zinawakwaza waandishi wa habari katika kufanya kazi zao kwa ufanisi. 

Imesema Wakati wanaingia mwaka huu wa 2024, waandishi na vyombo vya habari wana matumaini makubwa ya kuongezwa ushirikiano pamoja na kuzitafutia ufumbuzi wa 
haraka changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi za kila siku.

Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, vyombo vya habari, waandishi wa habari na wadau wa sekta hiyo pamoja na watetezi wa haki za binaadamu na utawala bora, wamekuwa wakipigia kelele kuwepo kwa mazingira mazuri/rafiki ya utendaji kazi.

Pamoja na hayo kamati hiyo imeendelea kwa kusema mazingira hayo huletwa na sheria iliyo rafiki ambayo hutoa hakikisho la kutumika kwa uhuru mpana wa kutoa maoni, na uhuru wa vyombo vyenyewe vya habari katika kutafuta, kuchakata na kutoa taarifa mbalimbali kwa jamii ikiwa ni jukumu mahsusi la vyombo vya habari kwa umma na taifa.


Walisema Sheria kuu ambazo zinahitaji kufanyiwa marekebisho ni pamoja na Sheria ya magazeti namba 5 ya mwaka 1988 iliofanyiwa marekebisho na sheria namba 8 ya mwaka 1997 pamoja na Sheria ya utangazaji namba ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho na Sheria namba 1 ya mwaka 2010.


Aidha, taarifa hiyo   tunapongeza na kuwashukuru wadau na Serikali kwa jinsi ilivyobeba ajenda hii  muhimu na kwa yake kupitia kauli na matamshi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na na Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi ambae alieleza wakati wa kutimiza siku 100 za Uraisi wake.

Hata hivyo kamati hiyo ilisema Kwa bahati mbaya hadi 
sasa sheria hizo hazijarekebishwa. 

Kwa nyakati tofauti tofauti Waziri waHabari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita pia amekuwa akieleza hamu hiyo ya Serikali ya kuwa na sheria mpya na nzuri.


"Kutokana na mtazamo huo wa kiuongozi, tumekuwa na matumaini ya kuona utekelezaji wa ahadi hiyo unafanywa kwa mtitiriko mzuri katika namna ambayo unafikia tamati kwa kupatikana sheria mpya ya habari badala ya sheria iliyopo sasa ambayo sio sisi wadau wala serikali yenyewe isiyotambua ukweli kwamba ni sheria ya muda mrefu na ambayo haiendani tena na ile dhamira njema ya kiongozi wa nchi yetu, na kadhalika, ikiwa isiyokidhi mazingira mapya yaliyochagizwana kasi ya ukuaji wa teknolojia, uwazi na 
uwajibikaji"  ilieleza sehemu ya taarifa hiyo


Kwa kuwa yamekuwepo maoni na mapendekezo mengi ya Waandishi wa Habari pamoja na Wadau wa Haki za Binaadamu, mapendekezo ambayo yapo mikononi mwa mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tunaaminiwakati umefika sasa wa kuendelea 
kufanyiwa kazi ili kuhakikisha lile lengo lililokusudiwa, linafikiwa kwa wakati muafaka.


Ni matamanio yetu kwamba mwaka huuwa 2024ndio mudasahihiwa kuona lengo la kupatikana kwa sheria mpya iliyo rafiki kwa kila upande, linafikiwa.Aidha wadau wa 
habari wataendelea kuwa tayari kutoa ushirikiano wa ainayoyote inapohitajika kwa ajili ya kutimiza lengo hilo.

Post a Comment

0 Comments