Ticker

6/recent/ticker-posts

Serikali Kuongeza Nguvu Miundombinu Sekta Ya Kilimo


Na Nafda Hindi:

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo ili kuleta tija katika sekta ya kilimo.

Akizinduwa maonyesho ya siku ya wakulima nane nane Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya maonyesho ya kilimo Dole Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya kiliomo ni muhimu mkubwa hivyo inahitaji kuwekewa miundo mbinu imara ili kuifikia dhana ya Mapinduzi ya kilimo.

Dkt. Mwinyi amesema kulingana na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema vijana na wanawake ni msingi imara kwa mfumo wa chakula inadhihirisha wazi nguvu kubwa na mchango wa wanawake na vijana kwa kumbuwa muamko wao ili kujenga Taifa lililo bora.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Wizara ya Kilimo zinaonesha kwamba 70% ya wakaazi wa Zanzibar wanategemea kilimo ili kuendesha maisha yao ya kawaida.

Hata hivyo katika kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo, Dk Mwinyi amesema utafiti unaonesha kilimo cha mbogamboga na matunda kimefanya vizuri kwa kuongeza uzalishaji kutoka tani 64 mwaka 2021 hadi tani 66 2022.

Mapema Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji na mifugo Mh Shaame Shamata Khamis amesema mafanikio katika sekta ya kilimo yamefikiwa kutokana na mashirikiano ya wananchi kuonesha jitihada mbali mbalo za kujikwammua na umaskini.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo Seif Shaaban amesema kwa sasa muamko ni mkubwa kwa jamii na zaidi ya washiriki mia mbili na sabiini na mbili watashiriki katika maonyesho ya siku ya wakulima (nane nane) kutoka Taasisi mbali mbali za Serikali, binafsi pamoja na wajasiamali 

Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa amesema ni vyema eneo la maonyesho ya siku ya wakulima kuboreshwa na kuwa la kisasa jambo ambalo lotasaidia wananchi kufika kwa urahisi na kunufaika na maonyesho hayo.

Katika maonyesho hayo wakulima wamepaza sauti zao kwa kusema licha ya kushiriki katika shughuli za kilimo kwa kujikwamua na umaskini bado wanakabiliwa na matatizo kadhaa yakiwemo soko la kuuzia bidhaa zao pamoja na pembejeo.

Maonesho ya siku ya wakulima Zanzibar hufanyika kila ifikapo tarehe 1Augosti ambapo kwa mwaka huu yamegharimu milioni mia tano na kumi na mbili hadi kukamilika kwake.

  

Post a Comment

0 Comments