Nafda Hindi, Zanzibar
VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuibua matatizo mbalimbali yanayohusiana na afya ya uzazi kwa wanawake na wasichana jambo ambalo husababisha wanawake wengi kutojiunga na huduma ya afya ya uzazi.
Akifungua mafunzo ya siku tatu kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA ZNZ, mjumbe wa bodi ya Chama hicho Shifaa Said Hassan, alisema ni wajibu kwa waandishi kufatilia na kuandika matatizo yanayowakabili wanawake hususani wanapotaka kujiunga na huduma hizo ili waweze kujua njia bora na salama.
“Licha ya kuwepo kwa sera na seheria zinazosisitiza umuhimu wa mwanamke kupata huduma hizo lakini inaonekana asilimiia kubwa ya kundi hilo hawana uelewa wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya huduma hiyo hivyo kupitia vyombo vya habari itakuwa chachu ya kuwaelekeza na kufikia malengo ya kuimarisha afya zao,”Shifaa Said, amesma.
Aidha aliwaomba waandishi wahabari kuwa kusikiliza kwa makini mafunzo wanayopata kwa lengo la kuyafanyia kazi ipasavyo ili yalete tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake mkufunzi na Mwandishi Mkongwe wa mafunzo hayo Salim Said Salim alisema wanawake wengi na watoto wanakosa haki zao za msingi ikiwemo kukosa lishe bora malezi ya pamoja baina ya mke na mume, hali ambayo husababisha jamii kukosa kizazi kisicho bora.
Amesema waandishi wahabari lazima wafatilie na kuibua ishu ambazo zinahusiana na haki ya afya ya uzazi na badala yake wasiridhike na kufunguliwa kwa vituo vya afya.
“Nawasisitiza waandishi wahabari kufanya uchunguzi juu ya huduma zinazotolewa kama kuna madaktari wa kutosha, dawa za kutosha ili kwenda sambamba na mahitaji ya wananchi katika kupata huduma bora,”Salim Said Salim,Mkufunzi.
Akiwasilisha mada ya afya ya Uzazi na malezi ya watoto katika Uislamu Mjumbe wa Baraza la Maulamaa kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibarm Sheikh Khamis Abdulhamid Khamis amesema katika kuwalea watoto ni jukumu la wazazi kuzingatia umri wa mtoto tokea siku anayozaliwa mpaka kufikia baleghe na kuendelea kujenga ukaribu na kuwafatilia katika nyendo zao.
‘’Katika malezi ya watoto, ni wajibu wa wazazi kushirikiana kwa pamoja kujuwa tabia za watoto wao. Watu wanaoshirkikana nao kama vile marafiki, ni lazima kuwachagulia marafiki wema, hii itawasaidia hata makuzi yao, na pia husaidia kuimarisha afya ya uzazi na malezi kwa mtoto kwa mujibu wa kitabu kitukufu cha qur ani kupitia aya mbali mbali za qurani,” Sheikh Khamis Abdulhamid.
Nae Mkufunzi wa magonjwa ya Uzazi na wanawake kutoka hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja Dk Ummulkulthum O.Hamad amesema waandishi wahabari kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu masuala ya haki ya afya ya uzazi,
“Katika jamii kuna shida bado Elimu ni ndogo kabisa kuhusu afya ya uzazi, ukizungumzia suala hili jamii yetu inadhani ni suala la wanawake pekee bali ni la linamgusa kila binadamu kwa sababu mtoto akizaliwa jambo la kwanza unaulizwa umepata mtoto gani? Badala ya kuuliza hali ya mama mtoto inaendeleaje, hapa ujuwe tayari jinsia imeanza" alisema Dk Ummulkulthum.
Nao waandishi wahabari wamesema watayatumia mafunzo waliyoyapata kwa kuandika habari na kutayarisha vipindi vinavyohusiana na haki ya afya ya uzazi kwa lengo la kutoa Elimu kwa jamii ili kuondokana na dhana potofu kwamba masuala haya yanamuhusu mwanamke pekee.
Washiriki wa mafunzo hayo wakieleza changamoto ziliyopo katika afya ya uzazi walisema ni pamoja na madaktari wanaotowa huduma hiyo kutokuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa sambamba na kutokuwa na uelewa juu ya baadhi ya huduma wanazizitoa
Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na tamwa zanzibar kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuielimisha jamii kuhusiana na afya ya uzazi.
0 Comments