JESHI la
polisi wilaya ya Kusini imedhamiria kuimarisha hali ya ulizi na usalama
wilayani humo kwa kuwashirikisha wanajamii ili kufikia lengo la kukataa uhalifu
kwa kila mwananchi.
Dhana hiyo imekuja kuongezwa kazi na kampeni maalumu ya ulinzi JIRANI ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti uhalifu ikiwemo makosa ja jinai.
Wakitoa ufafanuzi juu ya kampeni hiyo katika viwanja tofauti Inspekta Msaidizi wa Polisi Kulwa na Inspekta wa Polisi ambaye pia ni Mratibu wa Bonanza hilo Mtumwa Mussa Khamis wamesema ni Hali ya mwananchi kulinda eneo lake na la jirani yake Ili lisifanyiwe uhalifu.
Wamesema endapo majirani hawatoshirikiana katika ulinzi kuna uwezenano mkubwa kufanywa uharibifu wa Mali hivyo wametoa wite kwa majirani kutekeleza dhana hiyo ya ulinzi katika kuweka usalama wa mali zao.
Ikumbukwe wiki iliyopita Mratibu wa bonanza hilo
Inspekta wa polisi Mtumwa kwenye kipindi cha Zenj Sports kinachorushwa hewani
na kituo cha Redio cha Zenj FM alisema lengo kuu la bonanza hilo ni kutoa elimu
kwa vijana juu ya kujiepusha na makosa ya jinai.
Matokeo ya michezo ya leo:
Uwanja wa Kibuteni
Kizimkazi Dimbani 0-0 Mtende
Uwanja wa Jamuhuri Makunduchi
Nganani 4-1 Kibuteni
Ratiba ya michezo ya Kesho:
Uwanja wa Kibuteni
Muyuni “B” VS Kajengwa
Saa 10:00 Alaasiri
Uwanja wa Jamuhuri
Kizimkazi Mkunguni VS Kijini
Saa 10:00 Alaasiri
0 Comments