Ticker

6/recent/ticker-posts

Tatizo La Kukosekana Maji Safi Na Salama Jambiani Na Paje Lapatiwa Suluhisho

 


Wananchi wa maeneo ya Jambiani Paje na maeneo Jirani wanatarajiwa kuondokana  na  tatizo la ukosefu wa maji safi na salama  mara baada ya kukamilika  kwa zoezi la ufungaji wa vifaa vya kuongezea  nguvu za umeme katika visima  vya  Jambiani Kumbini na Paje.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini  Unguja Mhe Rashid Hadid Rashid ameyasema hayo wakati akifanya ziara na watendaji wa mamlaka ya  maji zawa, shirika la umeme ZECO, na uongozi wa wilaya  na jimbo ikiwa ni muendelezo wa taasisi hizo kufanya  ukaguzi katika vianzio vya maji ili kubaini matatizo yanayosababisha kukosekana kwa huduma hiyo kwa baadhi ya maeneo ya mkoa huo.

Amesema  mara baada ya kufanyika  ukaguzi na watendaji hao kumebainika  kueko kwa tatizo la umeme mdogo Pamoja na kutobolewa kwa miundo mbinu kiholela kwa shughuli za kilimo hivyo amewataka wananchi kuachana na tabia hiyo sambamba na kuwataka watendaji wa taasisi hizo kuharakisha zoezi la ufungaji wa vifaa hivyo ili wananchi waweze kuondokana na usumbufu wanaoupata hasa katika kipindi hichi ambacho tunaelekea na mwezi mtukufu wa Ramadhani.  

Nao wataalam  kutoka  mamlaka ya maji zawa mkurugenzi ufundi  injinia Hassan  khamis Hassan  na injinia wa zeco  Ali Kassim  wamesema watahakikisha wanalisimamia  zoezi hilo ili kuona  huduma hiyo inapatikanwa kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhan  huku wakiwasisitiza wananchi kuitunza  na kuilinda miundombinu ya huduma  hizo ili kuipunguzia hasara Serekali.

Nae kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Paje Mhe Jaffar Jussa Sanya  amesema uongozi wa jimbo hilo utaendelea na juhudi zake za kuzitafutia  ufumbuzi changamoto zinzowakabili wananchi  katika huduma muhimu ikiwemo maji, afya, na elimu.


Post a Comment

0 Comments