Ticker

6/recent/ticker-posts

“Waandishi Wa Habari Muna Wajibu Wa Kuzungumzia Haki Za Wanajamii” Dkt.Mzuri Issa

 Chama cha waandishiwa habari wanawake Tanzania TAMWA kwa upande wa Zanzibar kupitia kwa mkurugenzi wake Dkt. Mzuri Issa kimemesema kuna Umuhimu Mkubwa kwa Waandishi wa Habari kupewa Elimu juu ya kutambua Huduma Bora wanazostahiki kuzipata Wanajamii katika Kutekeleza Majuiumu yako ya Kila Siku.

 Akifungua Mafunzo ya Siku Nne kwa Waandishi wa Habari ya ushirikishwaji wa mwanamke katika uongozi yenye lengo la Kutambua Haki wanazostahiki Kupatiwa Wanajamii katika Kutekeleza Majukumu yao katika Shughuli za Maendeleo ya Jamii huko katika ukumbi wa chama hicho Tunguu amesema jamii inapaswa kufahamu Mwenendo na Taratibu za Kijamii zinazowazunguka Ikiwemo Suala la Kodi, Suala la Uchumi na Kutambua Sheria mbalimbali.

 Hivyo amewataka Waandishi wa Habari kufikisha Taaluma hiyo kwa Jamii ili Kusaidia Maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

 Mafunzo hayo ya Siku nne  yameandaliwa TAMWA-Zanzibar, ZAFELA, PEGAO, kwa Udhamini wa Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments