Makamu Wa Pili wa SMZ Mhe. Hemed Suleiman Abdula akihutubi kwaniaba ya Raisi Dkt. Mwinyi katika kongamano la wanawake wahasibu Tanzinia huko katika hoteli ya Verde Zanzibar. |
RAISI wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Ali Mwinyi amekipongeza Chama cha Wahasibu Wanawake
Tanzania (TAWCA) kwa jitihada zao katika kuandaa viongozi bora wanawake
wanaotoa mchango kwa maendeleo ya Taifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed
Suleiman Abdulla ameleza hayo kupitia Hotuba alioisoma kwa niaba ya Rais Dk.
Huseein Mwinyi katika ufunguzi wa kongamano la nne la uongozi la wanawake
wahasibu Tanzania (TAWCA) lililofanyika katika ukumbi wa Hotel Verde Mtoni Jijini
Zanzibar.
Mhe. Hemed amesema amefurahishwa na mikakati
iliowekwa na chama hicho katika kuhakikisha wanalisaidia taifa kwa kuandaa
viongozi mbali mbali wanawake ambao wamekuwa wakitoa mchango wao katika kukuza
Uchumi wa Nchi.
Makamu wa Pili wa Rais amesema kwamba Tanzania ina
viongozi wengi wakupigiwa mfano ambao wameweza kushika nafasi mbali mbali
kitaifa na kimataifa, kutokana na uwezo walionao wao. jambo ambalo limetoa
Imani kubwa kwa jamii kwa viongozi wanawake.
Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais
amewataka washiriki hao kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Serikali zote
mbili katika kupiga vita rushwa pamoja na vitendo vya ubadhirifu wa fedha
za umma.
Nae, Mwenyekti wa Chama cha Wahasibu Wanawke
Tanzania Dk. Neema Kiure Msussa, ameleza kuwa Chama hicho kimesajiliwa mwaka
2015 ambapo hadi sasa kina jumla ya wanachama 730.
Alieleza kuwa, TAWCA katika kuwawezesha
wajasirimali wanawake imesaidia jumla ya wanawake 101 kwa kuwapatia elimu
pamoja na kuwapa mafunzo na mitaji kwa ajili ya kuimarisha harakati zao za
kimaisha kupitia biashara.
Akiwasilisha salamu kutoka Hospitali ya Agakhan
katika kongamano hilo Dk. Erine Kitege alieleza kuwa katika Kongamano hilo
wataalamu kutoka Hospital hiyo watafanya vipimo vya saratani ya Shingo ya kizazi
na saratani ya matiti kutokana na kina mama kukumbwa na ugonjwa huo.
0 Comments