Ticker

6/recent/ticker-posts

Majina Ya Wahalifu Jimbo La Uzini Mikononi Mwa RC

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid


Serikali ya mkoa wa kusini unguja imesema itahakikisha inafanya uchunguzi juu ya  majina ya watu wa  shehia  nne za jimbo la  uzini yaliyofikishwa  ofisini kwake wakituhumiwa kujihusisha vitende mbalimbali vya kihalifu. 

Mkuu Wa Mkoa Wa Kusini Unguja  Rashid Hadid  Rashid  ametoa kauli hiyo huko katika Shehia  Kiboje Mkwajuni wakati alipokutana na wakaazi wa shehia nne za jimbo la uzini  kwa ajili yakusikiliza kero zinazowakabil katika vijiji vyao ambapo majina hayo yaliwasilishwa huku watuhumiwa wakituhumiwa kwa makosa ya udhalilishaji,uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevyapamoja na wizi wa mazao hivyo amesema endapo watabainika na kuwa na makosa hayo watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria za nchi.

“Tumeona majanga haya yanavyoongezeka siku hadi siku ila sasa tutahamia katika shehia hizi hivyo tushirikiane kutokomeza matendo haya” amesema Mhe. Hadid

Amesema  kukithiri kwa  vitendo hivyo ndani ya shehia hizo kumepelekea kuwepo kwa malalamiko  na kushindwa kufanya shughuli zao hali inayopelekea kurudisha nyuma shughuli zao mbalimbali za kiuchumi na maendeleo.

Viongozi  wa jimbo hilo Mbunge Mhe Khamis Hamza Chilo amesema kuzorota kwa upandikanaji haki kwa waathirika wa vitendo vya udhalilishaji ni kutokana na baadhi ya watu kutokutimizi majukumu yao kikamilifu hivyo amemuhakikishia mkuu wa mkoa kukaa na wanajamii ili kutafuta njia bora zitakazotokomeza vitendo hivyo.

“Unamkuta hasa mtoto kaharibiwa halafu bado unaendelea kupeleleza eti ushahidi haujakamilika unataka ushuhudie nini?” Alihoji Mbunge huyo

Kwa upande wao wakaazi wa shehia hizo wamesema kuongezeka kwa vitendo hivyo katika shehia zao kunatokana wananchi kutokuwa tayari kuwafichuwa wahalifu wa wanaofanya vitendo hivyo  huku wakiiomba serekali kuingilia kati  masuala hayo ili yaweze kupunguwa.

“Matendo haya yanachangiwa na sisi wenyewe kwa sababu katika vijiji tunajuwana lakini bado tunasitiriana au kuoneana muhali” alisema mmoja wa wanakijiji

Kikao hicho kilowashirikisha shehia nne za jimbo la uzini zikiwemo miwani, ghana, kiboje mkwajuni na mwembe shauri.

 

Post a Comment

0 Comments