Kamati Za wananchi zilizopewa dhamana Ya kusimamia
Miradi ya maendeleo Katika majimbo zimetakiwa kuweka utaratibu wa kusaidana
yanapotokea matatizo Ili kuhakikisha wanatoa Huduma nzuri kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya
huduma za jamii ambae pia ni diwani wa kuteuliwa manispaa ya Magharibi b, Thuwaiba Jeni
Pandu,alipokua katika ziara yake ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wa
shehia ya Pangawe wilaya ya magharibi B.
Amesema lengo la kufanya ziara hiyo ni baada
kupekea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kukosa huduma ya maji safi
na salama kwa muda mrefu jambo linalo walazimu kutumia gharama nyingi
kununua maji jambo linalodumaza hali za kiuchumi kwa wananchi hao.
Aidha amewataka wananchi kuwa nasubra katika kipindi
hichi kwani viongozi wa Jimbo watahakikisha wanatatua tatizo hilo ili kuona
furaha za wananchi hao zinaimarika.
Sambamba na hayo amesema viongozi wamekua wakijitahidi
kuhakikisha wanaondoa changamato ikiwa ni pamoja na kujenga visima
hivyo ni vyema kwa wanakamati kuwajibika ipasavyoa ili kuondolea usumbufu wanaopata
wananchi ikiwa ni kuhakikisha kuwa huduma zote za kijamii zinakuwa imara katika
maeneo yao.
Nao wanakamati wamesema tatizo kubwa lilopo ni
baadhi ya wananchi kushindwa kulipa ada hali inayo pelekea kushindwa kufanya
matengenezo pale linalopo tokezea tatizo katika miundombinu ya maji.
0 Comments