Waziri mteule wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mbunge wa Masasi, Mhe. Goodfrey Mwambe (shati ya bluu bahali) akipata maelezo ya bidhaa zinazozalishwa kutoka kwa mjasiliamali mdogo
Kuwepo kwa wajasiriamali wengi katika taifa ndipo
kunakopelekea maendeleo endelevu hususan katika sekta ya viwanda na biashara
nchini.
Hayo yalielezwa na waziri mteule wa wizara ya
viwanda na biashara Mhe, Geofrey Idelphonce Mwambe alipotembelea maonyesho ya tano ya
bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayoendelea huko katika uwanja wa maonyesho wa
Mwl J.K.Nyerere (SabaSaba).
Alisema
serikali ya Tanzania inathamini juhudi za wajasiriamali kwani wana mchango
mkubwa wa kuleta maendeleo chanya ktika taifa Zaidi katika Nyanja ya ajira
hivyo aliwahakikishia kufanya nao kazi pamoja na kuwaandalia mazingira wezeshi
ili kusudi waendelee na majukumu yao bila ya kuwepo na changamoto.
“serikali
itaendelea kuwapa msukumo ili tuone jitihada zenu katika kuleta mapinduzi ya
kiuchumi yanafanikiwa” alisema mteule huyo
Waziri mteule wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mbunge wa Masasi, Mhe. Goodfrey Mwambe (shati ya rangi buluu bahari) akipata maelezo ya bidhaa kutoka kwa afisa wa kiwanda cha Kahawa (Mbinga Coffee)
Alisema kuwa lengo la
kutembelea Maonesho hayo ni kujifunza,
kujionea bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu vya ndani, kujua bidhaa zinavyotengenezwa,
aina ya bidhaa hizo na kufahamu upatikanaji wa malighafi pamoja na kujua
muunganiko wa uzalishaji na upatikanaji wa masoko kwa bidhaa hizo.
“Nimepata faraja kuona mwamko mkubwa wa Watanzania kuweza kuzalisha bidhaa za Tanzania ambapo awali bidhaa hizo tulikuwa tunaagiza kutoka nje ya nchi, kupitia Maonesho nimeona dhamira yao na imenipa somo la kuona uhitaji wa uzalishaji mkubwa ili kuweza kusafirisha nje ya nchi” amesema Mhe Mwambe
Waziri mteule wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mbunge wa Masasi, Mhe. Goodfrey Mwambe (shati ya bluu bahali) akipata maelezo ya bidhaa zinazozalishwa kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam wakati alipotembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 -9 Desemba
Aliongezea kuwa nchi
ya Tanzania imeingia kwenye uchumi wa
kati, hivyo wajasiriamali wakiwezeshwa kwa kupata kipato kikubwa, wastani
wa mapato utaongezeka na kuwa juu hivyo juhudi ya pamoja ndani ya serikali
kuelekea mwaka 2025 nchi itaingia kwenye uchumi wa kipato cha juu utakaopelekea
kuboresha maisha ya Watanzania na kutengeneza uchumi wa viwanda ulio imara
pamoja na wenye muunganiko mzuri kati ya wajasiriamali wa kilimo, mifugo,
uvuvi, viwanda na masoko .
0 Comments