Nyota
huyo ambaye anamenyana na mzawa John Bocco anayekipiga ndani ya Simba kwenye
chati ya ufungaji ambapo amefunga mabao sita huku Bocco akiwa ni namba moja kwa
kufunga mabao yake saba ndani ya ligi kuu Tanzania bara.
Habari
zinaeleza kuwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze inahitaji mzawa
mmoja mwenye uwezo wa kucheka na nyavu ili awe mbadala wa Michael Sarpong
ambaye kasi yake ni ya kusuasua akiwa na mabao manne.
Kwa
upande wa Simba wao wanahitaji mbadala wa Charlse Ilanfya ambaye mambo kwake
yamekuwa magumu kwa kushindwa kuonyesha kile walichotarajia baada ya kuipata
saini yake kutoka ndani ya KMC.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mkuu wa Idara ya Mashindano ndani ya Gwambina FC, Mohamed Almas
maarufu kama Mtabora amesema kuwa bado hawajapokea ofa kwa sasa wanasubiri
dirisha dogo lifunguliwe kwanza.
"Kwa
sasa dirisha dogo la usajili bado hivyo hakuna ofa ya mchezaji wetu Meshack,
tunasubiri tuone itakuaje kama wanaweza kuja hilo ni jambo la kukaa
mezani," .
Nyota
mwenyewe Meshack amesema kuwa hana tatizo akipewa taarifa kuhusu kucheza katika
timu hizo kwa kuwa kazi yake ni mpira.
0 Comments