Ticker

6/recent/ticker-posts

"NINA IMANI NA UTENDAJIKAZI WA DKT. MWINYI" MAALIM SEIF

 


Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Taifa ambae pia ni makamu wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar Maalim, Seif Sharif Hamad amesema suala la cha ma hicho kuingia katika serikali yua umoja wa kitaifa liliamuliwa na wanachama wenyewe.

 

Akizungumza na wanachama wa chama hicho huko katika Afisi kuu za chama hicho Zanzibar, Vuga Mjni Unguja amesema suala hilo lilipitishwa kwa wanachama ili kutoa maoni yao juu ya jambo hilo ambapo idadi ya waliokubali kuingia katika serikali ya umoja wa kitaifa ilikuwa ni kubwa kulinganisha na wale waliokataa.

 

Hata hivyo Maalim, Seif amesikitishwa na baadhi ya kauli za miongoni mwa wanachana zinazomshutumu kuwa na malengo binafi juu ya kuingia kwake katika serikali hiyo.

 

Aidha Maalim Seif amesema chama cha ACT-Wazalendo kinaimani na utendajikazi wa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi ambapo watampa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha wanaondoa vitendo vya ubaguzi na ubadhirifu wa mali za umma.

 

Sambamba na hayo amesema katika nafasi za mawaziri ambazo zimebaki atapendekeza majina ya watu webye uwezo mkubwa na wanaoendana na kasi ya Dkt. Mwinyi ya kuwaletea wananchi maendeleo ya uhakika.

Ikumbukwe mnamo tarehe 5 mwezi huu kamati kuu ya chama hicho ilikutana na pitisha maazimio mbalimbali ikiwa moja ni kukubali kuingia katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Post a Comment

0 Comments