WANANCHI wametakiwa kuwa na tahadhari
kuhusu ujumbe unaosambazwa kwenye mtandao wa Facebook unaotumia jina la ‘Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa’ ukiwataka wajasiriamali watume pesa ili wapewe mkopo na
taasisi iliyojitambulisha kama Kassim Majaliwa Foundation, kwani mtandao huo ni
batili.
Katika taarifa iliyotolewa leo
Dicemba 8 na Ofisi ya waziri mkuu kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa Ujumbe huo unawataka wananchi
watume namba za vitambulisho vya kupiga kura ili waweze kupatiwa mkopo anaotaka
mkopaji ndani ya saa 24 kwa kutumia namba ambayo imesajiliwa kwa jina la Yunus
Milanzi.
Kufuatia kuwepo kwa kadhia hiyo Ofisi
ya Waziri Mkuu imekanusha kuwepo kwa taasisi hiyo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa hahusiki na Taasisi yoyote ya
utoaji wa mikopo.
Aidha taarifa imeendelea kusema kuwa Ofisi
ya Waziri Mkuu inafuatilia suala hilo kwa karibu ili kuwabaini wahusika wa
utapeli huo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
0 Comments