Ticker

6/recent/ticker-posts

KIKWETE ATOA DARASA NDOA YA MANARA


 

OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, siku ya jana amefunga ndoa na mkewe Naheeda, katika msikiti wa Masjid Maamur.

Katika Ndoa yake huyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, Sheikhe Mkuu wa mkoa wa Dar, Alhad Mussa Salum na watu wengine wengi maarufu.

Katika nasaha zake Raisi mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Kikwete alisema kuwa Haji alimfuata nyumbani na kumshirikisha jambo hilo kwa ajili ya ndoa na akamuahidi kuja.

Aidha Dkt. Kikwete alisema katika ndo hakuna ufundi isipokuwa jambo pekee na la muhimu ni kuvumiliana kutokana na kasoro za kila mwanandoa.

“Hakuna ufundi kwenye ndoa kikubwa ni kustahimiliana na kuvumiliana kwa kuwa hakuna ufundi katika ndoa” alisema Dkt. Kikwete

Vilevile Dkt. Kikwete aliendelea na nasaha zake kwa Wanandoa hao aliwataka wawe makini katika ndoa kwa kuwa na msimamo wa kuaminiana sambamba na kuweza kulea vyema vizazi vyao kwa maadili mema pale watakapojaaliwa kupata vizazi hivyo.

"Mnapaswa kuwa makini na kuskilizana katika ndoa, pia nakushauri ujue kwamba uwe na uvumilivu na kuona namna gani mnaweza kuleta watoto kwa kuulizana na kujua mambo yatakuaje”

Alisema katika suala hilo la kupata kizazi ni kazi ya Muumba mwenyewe hivyo wawe na subira hadi pale watakapojaliwa kupata kizazi.

"Baraka za Mungu kwa watoto ni zake ka kadri atakavyoamua, yale makundi yaache kwa kuwa kila mmoja anajua anachokipenda”

 

"Nilikuwa ninazungumza na mzee hapo nyuma akaniambia kwamba anahitaji wajukuu hivyo ni jambo la kheri na linahitaji subira kikubwa ninawapongeza katika hilo na ninaamini kwamba itakuwa kheri," amesema.

 

Post a Comment

0 Comments