Ticker

6/recent/ticker-posts

"JAMII ELEKEZENI NGUVU KATIKA KUJITOLEA" MRATIBU WA UNV TANZANIA

 

Jamii nchini imeshauriwa kuwa na muamko katika mambo ya kujitolea ili kuhakikisha mabadiliko ya kiuchumi na kujamii yanaimarika siku hadi siku.

Hayo yalielezwa na mratibu mkaazi wa shirika la kujitolea la  umoja wa mataifa la UNV anayefanya kazi zake nchini Tanzania, bwana Christian Mwamanga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habar huko katika hoteli ya Verde iliyopo Mtoni wilaya ya mjini unguja.

Alisema suala la kujitolea kwa wanajamii linachangia kwa kiasi kikubwa ukuwaji wa uchumi katika mataifa mbalimbali licha ya baadhi ya wanajamii wengi kutoitumia fursa ya kujitolea na badala yake wakiwa wameelekeza kufanya kazi zenye kuwapatia malipo jambo ambalo hurejesha nyuma jitihada za wanaojitolea.

“endapo jamii ikiw na muamko wa kujitolea tutapiga hatua kubwa ya maendeleo yetu tuwe wazalendo wa kujitolea tusitegemee sana kulipwa” Alisema Bwana Christian

Aidha alisema shirika la kujitolea duniani la UNV limekuwa likifanya mambo mengi kuzisaidia jamii ambapo alisema zaidi ya watu bilioni moja duniani wanafanya kazi za kujitolea huku asilimia 70 kati yao ni wale ambao wanafanya kazi katika sekta zisizo rasmi na asilimia 30 ndio ambao wanafanya kazi katika sekta zilizo rasmi.

“Kuna zaidi ya watu bilioni moja wanaojitolea duniani asilimia 70 kati yao wanafanya kazi katika sekta zisizo rasmi na asilimia 30 pekee ndio wanafanya kazi katika kekta zilizo rasmi” Aliongezea mratibu huyo

Alisema katika kipindi ambacho dunia imekumbwa na janga la COVID-19 watu wanaojitolea pia wamekubwa na janga hilo duniani kote ambapo licha ya kukumbwa kwao na janga hilo pia walichangia jitihada zao katika kupambana kikamilifu na janga hilo.

“Kwa mwaka huu dunia imekuwa na janga la virusi vya Corona kama watu tunaojitolea hatukunusurika” Alieleza

Alipozungumzia siku ya kujitolea duniani alisema kwa mwaka huu maadhimisho yake kitaifa yatafanyika Zanzibar katika kijiji cha Nungwi hapo kesho ambapo aliwataka wananchi wote kujitokeza kwa wngi katika maadhimisho ya sherehe hizo.


Alisema katika maadimisho hayo shughuli mbalimbali za kijamii zitakuwepo zoezi la uchangiaji damu wa hiari,mazungumzo ya kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika suala la kujitolea pamoja na michezo mbalimbali.

“Niseme tu kilele cha sherehe ya siku hii ya kujitolea duniani tukuwa na shughuli mbalimbali ambazo tutazitekeleza hapa Zanzibar tuchangia damu,tutazungumza mafanikio ya kujitolea pamoja na michezo” Alifafanua mratibu huyo

Siku ya kujitolea duniani husherehekewa duniani kote kila ifikapo tarehe tano Dicemba ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni "kwa pamoja tunaweza kuleta maendeleo endelevu Katika kujitolea.

Post a Comment

0 Comments