Na Ahmed Abdulla, Zanzibar
Katika zama za kidijitali, mitandao yakijamii imekuwa jukwaa lenye nguvu zaidi kwa viongozi, wanasiasa na wanaharakati.
Kwa wanawake, hususan wanaoishi katika jamii zenye mtazamo hafifu wa ushiriki wao katika uongozi, mitandao imekuwa njia ya kujitangaza, kujenga hoja, kuongeza uelewa wa jamii na kukusanya uungwaji mkono bila gharama kubwa.
Zanzibar nayo imekuwa sehemu ya mapinduzi haya, ambapo vijana na wanawake wanatumia Facebook, Instagram, X (Twitter), YouTube na TikTok kujipigia debe kwenye siasa, kuhamasisha jamii na kupigania usawa wa kijinsia.
Najjat Omar mtaalamu wa masuala ya mitandao ya kijamii alisema mitandao ya kijamii ni sehemu ya harakati za ukombozi katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
“Mitandao ya kijamii ni kura ya sauti kwa mwanamke inamuwezesha kuzungumza, kusikika na kushinda bila kuomba ruhusa.”
Alisema wanawake wengi hushindwa si kwa sababu hawana uwezo, bali kwa sababu hawajulikani hivyo mitandao ndio daraja la kujulikana katika harakati zao.
Pamoja na hayo aliwataka wanawake wagombea wa nafasi za uongozi kuendelea kujikita zaidi katika kulitumia jukwaa hilo kunadi sera zao na kujitangaza na badala yake kuacha tabia ya kujitangaza katika mambo yasiyo ya msingi.
Halima Ibrahim Mohd msemaji wa sekta ya maendeleo ya wanawake na watoto kupiyia chma cha Act wazalendo alisema wa wanawake kutukutumia mitandao ya kijamii kama jukwaa la kugombea nafasi za uongozi ni
Upinzani mkubwa unaotokana na imani za kifasihi kwamba mwanamke siyo mzuri katika uongozi wa kijamii.
Alisema aliweza kutumia mitandao ya kijamii kuonyesha shughuli za maendeleo, kusimamia miradi ya kijamii na kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi
“Mtandaoni niliwaonyesha kazi, ndipo wakaniamini,mwanamke akikaziwa, aoneshe kazi, sio
Abdalla Abeid mkurugenzi wa shirika la vijana la kupambana na changamoto za vijana ZAFAYCO ni kijana anayejulikana kwenye mtandao wa X kwa kupigania haki za wanawake kuingia kwenye uongozi.
Alisema mitandao ya kijamii ina nafasi kubwa na fursa nzuri kwa vijana katika kunadi sera zao na nia zao za kugombea nafasi za uongozi ili kuweza kufikia ndoto zao na usawa wa kijinsia kufikia asilimia 50 kwa 50 katika nafasi za uongozi.
“Wanawake siyo wapinzani wetu kwenye uongozi, ni washirika wa maendeleo. Tukiwanyima uongozi. “
Katika kuhakikisha wanawake wanagikia malengo yao ya kuwa viongozi bora katika nchi cmChqma cha wandishi wa Habari wanawake Tanzania (TAMWA ZNZ) kimekuwa mstari wa mbele kuwahamsisha wanawake waweze kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii kama fursa ambazo zitaketa mafanikio ya haraka
Mratibu wa mradi wa kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi Sabrina Yussuf Mwintanga alisema imekuwa nguzo muhimu na imara katika kuwafundisha wanawake jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kwa kunadi sera zao na kujitanga kwao.
“Hakuna usawa wa kijinsia bila ushiriki wa wanawake kwenye maamuzi. Teknolojia imefungua milango, sisi tunahakikisha wanavaa uwezo wa kuyapita.”
Maulid Hassan Zidi diwani wa viti maalum wilaya ya Kusini Unguja kupitia chama cha Mapinduzi CCM alisema kuwa mitandao ya kijamii imekuwa silaha muhimu kwa wanawake wanaotamani kugombea nafasi za uongozi, kwa sababu inawawezesha kufikisha sera na mawazo yao moja kwa moja kwa wananchi bila kupitia vichujio vya vyombo vya habari au upendeleo wa kisiasa.
Alisema kuwa majukwaa kama Facebook na Instagram yanawapa wanawake nafasi ya kutengeneza taswira yao ya uongozi, kuonyesha kazi walizowahi kufanya, na kuwahamasisha wapiga kura kuamini uwezo wao.
“Kwa mtazamo wangu , wanawake wanapoitumia mitandao kwa weledi, wanaongeza kujiamini na kuonekana zaidi katika harakati za kisiasa.”alieleza
Kwa upande wake, Rahima Said Abdalla mgombea wa uwakilishi jimbo la mwanakwerekwe alisema anaona kuwa mitandao ya kijamii imekuwa daraja la ushirikiano na ushawishi wakati wa kampeni za uchaguzi.
Alifafanua kuwa wanawake wengi waliokuwa hawana uwezo wa kifedha kwa ajili ya kampeni za gharama kubwa sasa wanaweza kujitambulisha kwa video fupi, chati za sera, mijadala ya moja kwa moja na makundi ya mawasiliano mtandaoni.
Alisema anaamini kwamba inapotumiwa kwa nidhamu, utafiti na ubunifu, mitandao inajenga jamii inayotambua uwezo wa mwanamke na inapunguza changamoto za ubaguzi wa kijinsia katika siasa.
“Mitandao ya kijamii ni nguvu ya mwanamke mgombea haimuhitaji kuwa tajiri ili kusikika, inamhitaji kuwa na taarifa sahihi na ujumbe wenye maono.” Alieleza.
Kwa mtazamo huo, mitandao ya kijamii imegeuka kuwa nguzo muhimu ya kuharakisha maendeleo ya usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.
Ili wanawake waendelee kunufaika na teknolojia hii, ni muhimu kupewa mafunzo, kuungwa mkono na kulindwa dhidi ya ukatili wa kimtandao ili sauti zao zisinyamazishwe.
Kadiri wanawake wanavyoitumia mitandao kwa weledi, ndivyo jamii inavyopata viongozi wabunifu, wenye dira na wanaoweza kutetea maendeleo ya wote.
Hivyo, mitandao si tu chombo cha mawasiliano, bali ni daraja la mabadiliko ya kweli katika uongozi wa wanawake.

.jpeg)
0 Comments